Mifuko ya Jamii iwafikie wajasiriamali vijijini

vijini kiNdugu Mhariri,

Mabadiliko ya sheria katika sekta ya hifadhi ya jamii Tanzania yanapokelewa kwa furaha kubwa na wananchi wa kawaida.

Sheria hiyo inawaruhusu mifuko hiyo kupanua zaidi wigo wa wanachama wake ambapo mtu yeyote, mwenye umri usiopungua miaka 18 anaweza kuwa mwanachama wa mifuko hiyo.

 

Kwa maoni yangu azma hiyo njema haitaweza kuzaa matunda mema kwa kiasi kikubwa kama zilivyotarajiwa, kwa sababu ya umangimeza uliokithiri miongoni mwa watendaji wa mifuko hiyo.

 

Mimi nilitarajia baada ya kupitishwa sheria hiyo wafanyakazi wa mifuko hiyo wangetoka maofisini, na huingia mitaani na vijijini waliko wananchi na kuwaelimisha na kuwahamasisha  ili waweze kujiunga kwa manufaa yao ya uzeeni.


Tunachokishuhudia sasa ni matangazo ya muda tu katika televisheni na baadala ya hapo wananyamaza. Wakati mwingine wanatutaka sisi wananchi tuangalie katika tovuti zao, wakidai eti humo kuna taarifa mbalimbali kwa wanachama na habari mpya zinazojitokeza mara kwa mara.


Wafanyakazi na watendaji hao ni Watanzania wenzetu wanaoelewafika kuwa asilimia 85 ya Watanzania, wanahishi vijijini ambako hakuna vyombo hivyo vya mawasiliano ya teknolojia ya kisasa, Je, wakulima, wajasiriamali na mtu yeyote aliyejiajiri mwenyewe watafikiwaje na huduma hiyo muhimu sana?


Napendekeza mifuko hiyo itenge katika bajeti zake za kila mwaka fedha za vipindi vya kudumu, katika redio na televisheni vya muda wa masaa 2 kila mfuko kwa wiki, kuwaelimisha umuhimu wa kuwa mwanachama wa mpango wa hiari.


Vile vile fedha nyingi sana za kuwawezesha wafanyakazi kwenda vijijini kwa wakulima

Lazima mifuko ielewe kuwa masuala haya ni mapya sana kwa wananchi wengi, hiyo inahitajika kufanya kazi ya ziada na ya kudumu kufanikisha suala hilo. Ni jambo la kusikitisha sana kuona nchi yenye nguvu kazi ya watu 18 millioni, mifuko ya hifadhi ya jamii inao wanachama wasiofikia hata million 3

Jeanster Elizabeth

P.O.Box Private Bag

Mwanza