Burudani

SKIIBII kafufuka baada ya kujiua kimuziki 

‘Hivi ndivyo mtu mashuhuri hufanya’. Ni jina la wimbo wa msanii wa Nigeria, Abbey Elias, maarufu kama Skiibii Mayana ama Swaggerlee, unaomtambulisha katika soko la muziki nchini humo na pande za dunia kwa sasa. Pamoja na umaarufu ambao umeanza kumvaa kijana huyu kwa sasa, mwaka 2015 hatasahaulika kwa mbinu yake ya kuusaka umaarufu kimuziki kwa kujitengenezea kifo na kutangazwa kwa ...

Read More »

V.MONEY unakua kimuziki na kuikuza sanaa yako

Sikio halilali njaa, wapenzi wa muziki wa Bongo Fleva baada ya kukanyaga na kutimua vumbi mitaani kwa nyimbo za vijana wa kundi la Wasafi (WCB) sasa ni muda wa Vanessa Mdee, maarufu kama Cash Madame na wimbo wake wa ‘Moyo’. Vanessa Mdee ambaye kwa mashabiki wake anafahamika zaidi kama V. Money, ameachia wimbo wa ‘Moyo’ wiki iliyopita ukiwa ni sehemu ...

Read More »

‘Matusi’ hayakwepeki Bongo Fleva?

Kumekuwa na malalamiko yanayozidi kushika kasi kutoka kwa wadau wa soko la muziki wa Bongo Fleva siku za hivi karibuni, kwamba nyimbo nyingi zinazotungwa na kuimbwa na wasanii wa muziki huo zimekuwa na kasoro za kimaadili, hazina viwango vya kutosha vya ubunifu na kubwa zaidi, zimesheheni lugha ya ‘matusi’. Hiyo ni mitazamo ya wadau hao ingawa kwa upande mwingine huenda ...

Read More »

Miaka mitatu baada ya kifo cha Papa Wemba

Miaka mitatu imetimia tangu mwanamuziki nguli, Papa Wemba, kufariki dunia. Ilikuwa mithili ya simulizi za ‘Alinacha’ asubuhi ya Jumapili Aprili 24, mwaka 2016, kuzagaa kwa taarifa za kifo cha mtunzi na mwimbaji mkongwe, Papa Wemba, kwamba amefariki dunia. Taarifa hizo zilieleza kwamba nguli huyo alianguka jukwaani akiwa anatumbuiza jijini Abidjan, nchini Ivory Coast katika tamasha la muziki la FEMUA. Baadhi ya ...

Read More »

Umri mdogo sifa kibao

Sifa kubwa alizonazo Aslay ni ule uwezo wa kutunga, kuimba na kurekodi nyimbo nyingi kwa kipindi kifupi. Aslay ni msanii wa kizazi kipya ambaye tungo zake zimekuwa zikiwakuna wapenzi wa muziki huo, ndani na nje ya nchi. Nyimbo za kijana huyo mdogo zimejikita zaidi katika mapenzi. Majina yake kamili ni Isihaka Nassoro, alizaliwa Mei 6, 1995, akapata elimu ya msingi ...

Read More »

‘Mmasai wa kwanza kupiga dansi’ (3)

Wimbo mwingine uliotia fora wakati huo ni ‘Bide’, alitunga na kuimba kwa lugha ya Kipogoro. Juma Ubao aliamua kupumzika mambo ya muziki kwa kipindi kifupi. Atumia muda huo wa mapumziko kwenda kusoma  masomo ya jioni akiwa na lengo la kuendeleza elimu yake. Alisoma masomo ya Uhasibu na Biashara ambako aliweza kupata cheti. Cheti chake kilimpa nafasi ya kupata ajira katika ...

Read More »

Buriani Lutumba Simaro Massiya

Lutumba Simaro Massiya aliyekuwa mtunzi na mcharazaji maalumu wa gitaa la ‘rhythm’ katika bendi za T.P. OK Jazz na Bana OK, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amefariki dunia Machi 30, mwaka huu katika Jiji la Paris, Ufaransa. Taarifa hiyo ilitangazwa na mwanawe wa kiume, Simon Lutumba, kutoka jijini Paris, kwamba baba yake Lutumba alifariki dunia akiwa na umri wa ...

Read More »

Diamond Plutnumz shujaa asiyechoka

Msanii wa kizazi kipya, Diamond Platnumz (pichani), ambaye ‘nyota’ yake inaendelea kung’aa kwa kuingiza pesa lukuki kutoka katika maonyesho yake amekuwa akipata mialiko mingi ndani na nje ya nchi, ambako hulipwa ‘kitita’ kizuri cha pesa. Mara baada ya kuzaliwa Oktoba 2, 1989 katika Hospitali ya Amana, jijini Dar es Salaam, alipewa majina ya Nasibu Abdul Juma. Kwa bahati mbaya hakupata ...

Read More »

P-Square wana utajiri wa kutisha

Wapenzi wa muziki wa kizazi kipya duniani, hasa Afrika, kundi la P-Square si geni masikioni mwao kutokana na kazi zake kukubalika katika makundi mbalimbali. Vijana hao wawili, ambao ni mapacha kutoka nchini Nigeria, Peter Okoye na Paul Okoye, wanaunda kundi maarufu linalojulikana kama P-Square. Mapacha hao nje ya muziki wanafanya biashara. Peter na Paul wamezaliwa jijini Lagos, nchini Nigeria, miaka ...

Read More »

Kipanya: Nilikotoka

Mchora katuni maarufu, Ally Masoud (Masoud Kipanya), amesema hataogopa kumchora rais wa nchi kwa kuwa havunji sheria na kwamba uchoraji wa katuni umedumu kwa muda mrefu duniani kote. Kipanya licha ya kuwa ni mchoraji wa katuni, pia ni mtangazaji wa kituo cha redio na televisheni, amewahi kuwa mhariri msanifu wa magazeti ya katuni. Pia alikuwa mhariri na mchoraji wa Gazeti la ...

Read More »

Pumzika kwa amani Oliver Mtukudzi

Mwanamuziki nguli wa muziki wa Jazz kutoka Zimbabwe, Oliver Mtukudzi ‘Tuku’(pichani juu), amefariki dunia wiki iliyopita katika Hospitali ya Avenues jijini Harare akiwa na umri wa miaka 66. Tuku alilazwa hospitalini hapo baada ya kuugua kwa muda mrefu. Kabla hajalazwa mwanamuziki huyo alikuwa katika ziara nchi mbalimbali duniani. Alilazimika kukatisha ziara yake kutokana na maradhi yaliyokuwa yanamsumbua. Tuku amefariki dunia ikiwa ...

Read More »

MAAJABU YA DK. REMY ONGALA (1)

Kama kuna mwanamuziki ambaye hawezi kusahaulika katika kumbukumbu za wapenda muziki ni Dk. Remmy Ongalla. Desemba 13, 2018 alitimiza miaka minane tangu afariki dunia. Alifariki dunia usiku wa kuamkia Jumatatu ya Desemba 13, 2010 nyumbani kwake Sinza, jijini Dar es Salaam. Ilikuwa ni siku ya majonzi kwa wapenzi wa muziki wa dansi Tanzania, Afrika Mashariki na ulimwenguni kwa ujumla baada ...

Read More »

Tumkumbuke nguli Shakila Binti Said (1)

Ni zaidi ya miaka miwili tangu atutoke Shakila Binti Said aliyekuwa nguli katika miondoko ya muziki wa taarabu humu nchini na Afrika Mashariki na Kati kwa ujumla. Wakati wa uhai wake, aliweza kuonyesha umahiri wake wa utunzi na uimbaji wa taarabu katika bendi zote alizowahi kuzitumikia. Shakila alifariki dunia ghafla, ambapo binti yake wa mwisho aitwaye Shani, alisikika kupitia vyombo mbalimbali ...

Read More »

Mkasa wa 2Pac Shakur Malaysia (2)

Tupac alilelewa katika mazingira magumu, jamii yake ilimpatia jina la ‘Black Prince’ kwa kuwa mama yake alimpenda mtoto wake. Tupac alikulia katika mazingira ya ‘kitemi’ kutokana na kushindwa kupata malezi bora, huku mama yake akishindwa kuwa karibu ili kumlea mtoto wake, ingawa alimpenda sana. Alikuwa akimsumbua sana mama yake kuhusu kumjua baba yake na mama huyo hakuwa na jibu la kuweza kumridhisha zaidi ya kumwambia ...

Read More »

Werrason alivyoitosa Wenge Musica (2)

Vijana wengi wa kizazi kipya cha muziki wa Kongo waliowahi kupitia kwa Werrason ni Ferre Gola, Heritier Watanabe, Fabregas, Robinho Mundibu, Bill Clinton, Celeo Scram, Brigade, Capuccino le Beau Gars, Didier Lacoste na Flamme Kapaya. Tangu mwaka 2000, Werrason anamiliki Shirika lenye majina ya Werrason Fondation, ambalo hutoa misaada zaidi kwa watoto yatima 400. Kupitia misaada hiyo Werrason ametokea kupendwa na ...

Read More »

Werrason alivyoitosa Wenge Musica

Na Moshy Kiyungi   Mwanamuziki, Noel Ngiama Makanda ‘Werrason’, aliamua kuikacha bendi yake ya Wenge Musica BCBG, akaamua kuunda kikosi chake cha Wenge Musica Maison Mere. Amejizolea sifa lukuki kufuatia ubunifu alionao na tabia yake ya ukuzaji wa vipaji pamoja na kasuka kikosi cha vijana chipukizi. Werrason alizaliwa Desemba 25, 1965 katika mji wa Kikwit,  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Alitanguliwa ...

Read More »

Samatta mguu sawa!

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Mbwana Ally Samatta, amekuwa lulu kwa klabu tatu za nchini Uingereza. Samatta yuko mguu sawa akisubiri Everton wazidi ‘kujikoki’. Tetesi zinasema nyota huyo anasakwa na West Ham United – ‘Wagonga Nyundo wa London’ , Everton na Burnley. Samatta, 25, maarufu kama ‘Samagoal’ nyota yake imeng’aa sana akichezea Klabu ya KRC Genk, ...

Read More »

Msimbazi ni majonzi

Wanachama na wapenzi wa Klabu ya Soka ya Simba ya Dar es Salaam, pamoja na wapenzi wa soka ndani na nje ya nchi wako kwenye majonzi makubwa baada ya kutekwa kwa mfadhili na mwekezaji mkuu wa klabu hiyo, Mohammed Dewji (Mo). Tangu taarifa za kutekwa kwake zianze kuvuma asubuhi ya Oktoba 11, mwaka huu, wanachama na wapenzi wa Simba wamekuwa ...

Read More »

Mourinho, mwisho wa enzi!

NA MWANDISHI WETU Alexis Sanchez anaweza kuwa ameokoa kibarua cha Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho, kufukuzwa mapema wiki hii baada ya kuwafunga Newcastle United 3-2 mwishoni mwa wiki. Endapo Jose Mourinho ‘The Special One’ atafungashiwa virago, Meneja wa Tottenham, raia wa Argentina, Mauricio Pochettino, anatajwa kurithi mikoba yake. Mourinho amekalia kuti kavu kutokana na timu yake ya Man United kutofanya ...

Read More »

SAM MANGWANA Mwanamuziki asiyechuja

NA MOSHY KIYUNGI Jina la Sam Mangwana si geni masikioni mwa wapenzi wa muziki wa dansi Afrika Mashariki na Kati. Ni mwanamuziki mwenye vipaji vya utungaji na kuimba nyimbo za muziki wa dansi akitokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Mangwana alizaliwa Februari 21, 1945 katika mji wa Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Wazazi wake walikuwa wahamiaji ambapo baba yake ...

Read More »

Mbilia Bel astaafu muziki

NA MOSHY KIYUNGI Tabora Mwimbaji mkongwe wa muziki wa Kilingala na Kifaransa, Mbilia Bel, amestaafu rasmi muziki Januari mwaka jana. Mwana mama huyo mapema Januari 2017, alitangaza kustaafu kwake wakati akisherehekea miaka 40 kwenye muziki, pia siku yake ya kuzaliwa kwa kutimiza miaka 58. Mbilia mwenye umri wa miaka 59, alianza kujiingiza kwenye kazi ya muziki akiwa na umri wa ...

Read More »

Queen Elizabeth Aibuka Mshindi wa Miss Tanzania 2018

Shindano la Miss Tanzania 2018 lilofanyika usiku wa Jumamosi Septemba 8, 2018 na kushuhudia Queen Elizabeth kuibuka na ushindi katika mshindano hayo. Queen alisema “Nafurahia kushinda taji ili najisikia vizuri sana asante Tanzania” akiongeza “ukiwa kama mrembo lazima ujiandae kama unavyoona warembo ni wazuri sio kwamba ni wazuri kumuonekano tu hata kichwani pia wako vizuri” na miongoni  katika fainali hiyo  Waziri ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons