page za ndani

Watoto wa Afrika tunaona au tunaonwa? (2)

Kuanguka kwa zama za ukoloni na ukoloni mkongwe kumetoa nafasi kwa ukoloni mamboleo na ubeberu kutamalaki Afrika. Watoto wa Afrika hatuna budi kuona kwa undani mifumo miwili hii inayotamalaki inakatishwa na kufutwa. Watoto wale (waliopita) wa Afrika waliona athari na madhara ya ukoloni na ukoloni mkongwe. Wakaung’oa. Leo Afrika iko huru. Je, watoto hawa (sisi) wa Afrika wanaona athari na ...

Read More »

Sauti ya Hemed Maneti bado inasisimua

NA MOSHY KIYUNGI TABORA Sauti ya Hemed Maneti ‘Chiriku’ kila isikikavyo kupitia redio, nyoyo za baadhi ya wapenzi wa muziki wa dansi hupatwa na simanzi kubwa. Nguli huyo alifariki dunia Mei 31, 1991 akiwa katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam ambako alikuwa amelazwa baada ya kuugua kwa muda mrefu. Mwili wa Maneti ulizikwa kijijini kwake ukisindikizwa na umati ...

Read More »

Ujamaa… (13)

Ndiyo kusema kwamba elimu inayotolewa sasa ni kwa ajili ya wachache tu wenye uwezo wa mitihani kuwazidi wengine; inawafanya wale wanaofanikiwa wajione kuwa wakubwa, na kuwafanya wale walio wengi wakitamani kitu ambacho hawatakipata daima. Inawafanya walio wengi wajifikirie kuwa wanyonge, na kwa hiyo hawawezi kuunda wala taifa la usawa tunalotaka kulijenga wala fikara zinazoelekea kwenye taifa lenye usawa. Kinyume chake, ...

Read More »

Waziri Kabudi

Wiki iliyopita Waziri wa Sheria na Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi, akiwa Marekani aliwapa darasa wana- diaspora kuhusu mambo mazito ya historia yetu na mambo yanayofanywa na serikali, cha kushangaza kilichotiliwa mkazo ni swali lililoulizwa kuhusu Tundu Lissu tu. Watanzania tubadilike. Msomaji wa JAMHURI, 0682874626 CCM iwe makini CCM iwe makini, wale iliowaita mafisadi wanarudi kiaina kwa kile wanachodai kuridhishwa na ...

Read More »

Waziri Lugola fika Zanzibar majipu ni mengi hayana mtumbuaji

Mhariri, kwanza nakupongeza kwa uzalendo wa kuichapa barua hii. Sababu kubwa ya kuandika andiko hili ni kumuomba Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, afike huku kwetu Zanzibar kujionea makosa ya barabarani yanayofanywa kwa makusudi bila kuchukuliwa hatua. Sitanii. Ukiwa barabarani kila dakika utaona daladala au gari la abiria lililozidisha abiria kupita idadi iliyoandikwa ubavuni kwa dereva. ...

Read More »

Mafanikio, changamoto Chuo Kikuu Huria

Mafanikio, changamoto Chuo Kikuu Huria Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Profesa Elifas Bisanda, amezungumza na Gazeti la JAMHURI kuhusu historia, mafanikio, changamoto na hatima ya chuo hicho. Mwandishi MANYERERE JACKTON, aliyezungumza naye, analeta maelezo ya Profesa Bisanda neno kwa neno. Endelea… Umuhimu wa kozi ya ‘foundation’ Kozi ya foundation ilianzishwa mwaka 1994/1995 na iliwawezesha wale ambao ...

Read More »

Mafanikio yoyote yana sababu (39)

Na Pd. Dk. Faustin Kamugisha Kwenda maili moja zaidi ni sababu ya mafanikio. Kufanya jambo zaidi ni sababu ya mafanikio. “Hakuna msongamano wa magari kwenye maili moja zaidi,” alisema Zig Ziglar. Maili moja zaidi haina umati wa watu. Maana yake ni kuwa kuna watu wachache wanaofanya mambo zaidi ya yanayotakiwa. “Mafanikio yanaanzia kwenye maili moja zaidi,” alisema Yulkan Shirlk. Mtu ...

Read More »

Shairi: Msiba wa Taifa

1: Sioni pa kuanzia, Kueleza taarifa, Nchi yetu Tanzania, Imekumbwa na maafa, Taifa zima twalia, Ni msiba wa taifa, Watu mia na zaidi, Leo tumewapoteza. 2: Raia kwa wanafunzi, Na wazazi kwa watoto, Wametujaza simanzi, Na mili kuwa mizito, Mili imeshika ganzi, Ni kwa hili jambo zito, Jamani watanzania, Tuwaombee wenzetu. 3: Tumeumbiwa upofu, Kifo kwetu bado fumbo, Ijapo tunayo ...

Read More »

Ajali ya mv Nyerere: tutajifunza lini?

Jambo ambalo si rahisi kuacha kulitaja ni hali duni ya usalama inayowakabili watumiaji wa vyombo vya usafirishaji kutokana na kujirudia kwa ajali mbalimbali. Watanzania tumo kwenye maombolezo ya vifo na hasara iliyotokana na ajali ya hivi karibuni ya mv Nyerere, kivuko kinachohudumia wakazi wa Kisiwa cha Ukara, Wilaya ya Ukerewe. Naandika makala hii ikiwa tayari imeopolewa miili zaidi ya 100 ...

Read More »

Man City yachekelea faida

Manchester, Uingereza Mabingwa wa Ligi Kuu nchini Uingereza, Klabu ya Manchester City, wametangaza kupata faida ya kiasi cha pauni milioni 500.5 sawa na Sh bilioni 1.5 kwa msimu wa 2017/18 na kuvunja rekodi ya mapato tangu kuanzishwa kwa klabu hiyo mwaka 1880. Pia klabu hiyo imetangaza kuwa tangu kuwasili klabuni hapo kwa Kocha wake, Pep Guardiola, wamefanikiwa kupunguza idadi ya ...

Read More »

Bilionea Mjapani kwenda kutalii mwezini

  Kampuni ya tajiri maarufu, Elon Musk, ya SpaceX imetangaza nani atakuwa abiria wake wa kwanza, mtalii, ambaye atasafirishwa kwenda kuuzunguka mwezi. Mtalii huyo atakuwa ni bilionea Mjapani Yusaku Maezawa, 42, ambaye pia ni mjasiriamali na mwenye biashara kubwa ya uuzaji wa mitindo ya mavazi na ubunifu kupitia mtandao. Mwenyewe ametangaza: “Nimeamua kwenda mwezini.” Anatarajiwa kusafiri kwa kutumia chombo cha ...

Read More »

MV Nyerere imeamsha uchungu

MV Nyerere imeamsha uchungu Na Deodatus Balile Ajali ya MV Nyerere iliyotokea Septemba 20, 2018 katika Ziwa Victoria imeamsha uchungu wa wakazi wa Kanda ya Ziwa. Imenikumbusha siku ya Jumanne ya Mei 21, mwaka 1996 ilipozama meli ya MV Bukoba na kuua watu zaidi ya 800. Takwimu zinatofautiana. Wapo wanaosema walikufa watu 1,000 na wengine wanasema walikufa 800. Vivyo hivyo ...

Read More »

Serikali ‘isiwaue’ wafanyabiashara Kariakoo

NA MWANDISHI WETU DAR ES SALAM Wiki iliyopita kimefanyika kikao baina ya jumuiya ya wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo na mawaziri watatu; Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwezeshaji, Charles Mwijage; Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isaac Kamwelwe. Kikao hicho kimefanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam huku ...

Read More »

Dar yaongoza ajali, Tabora mauaji – LHRC

DAR ES SALAAM NA CATHERINE LUCAS Ofisa Mipango Msaidizi, Masoko na Haki za Binadamu wa Kituo cha Haki za Binadamu na Msaada wa Kisheria (LHRC), Tito Magoti, amesema Jiji la Dar es Salaam linaongoza kwa matukio ya ajali za barabarani. Akizungumza na JAMHURI, Magoti amesema licha ya takwimu kuonyesha jiji hilo linaongoza kwa ajali na wingi wa askari wa usalama ...

Read More »

Muhimbili wanatekeleza kwa vitendo agizo la JPM

NA ANGELA KIWIA Hospitali ya Taifa Muhimbili imetekeleza kwa vitendo agizo la Rais Dk. John Magufuli la kubuni mkakati wa kupunguza idadi ya wagonjwa wanaotibiwa nje ya nchi. JAMHURI limefanya mahojiano maalumu na Ofisa Habari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminiel Aligaesha, kuhusiana na utekelezaji wa agizo hilo la rais. JAMHURI: Utekelezaji wa agizo la rais umefikia wapi? Aminiel: Kwanza ...

Read More »

Hatari mpya

*Wataalamu waonya usafiri Ziwa Victoria si salama *Wahoji nchi ilivyojiandaa kukabili majanga mapya *Wengi wakumbuka yaliyotokea kwa MV Bukoba *Waziri Mkuu aeleza ya moyoni, kivuko kuvutwa Na Mwandishi Wetu, Ukara Wahandisi na wataalamu wa majanga wamesema Tanzania inakabiliwa na hatari kubwa mbele ya safari iwapo serikali haitafanya uamuzi mzito katika usafiri wa majini, JAMHURI limeelezwa. Wakizungumza na JAMHURI kwa nyakati ...

Read More »

Mjue Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka

  DAR E SALAAM NA MWANDISHI WETU, Akiwa ziarani katika Mkoa wa Simiyu, Rais John Magufuli, alimsifu Mkuu wa Mkoa huo, Anthony Mtaka, na kumtaja kama kiongozi mahiri aliyefanya mambo mengi, mazuri kwa muda mfupi. Akasema awali alipopendekeza jina la Mtaka, aliambiwa (vetting) kuwa kiongozi huyo kijana hafai hata kuwa Mkuu wa Wilaya (DC), lakini kazi alizofanya zimemfanya awe RC ...

Read More »

Ndugu Rais Katibu Mkuu CCM awe tumaini letu

Ndugu Rais, ni lini mwokozi wangu atapita kwangu nami nipate kuligusa pindo la vazi lake ili haya ninayowalilia waja wake yafike mwisho? Maskini aliye na raha ya Mungu ana raha ya milele! Chama Cha Mapinduzi kimepata Katibu Mkuu mpya. Na awe tumaini la wenye mioyo iliyopondekapondeka! Katibu Mkuu weka akilini kuwa, umeteuliwa kushika nafasi hiyo kutokana na vile ulivyo sasa. ...

Read More »

MAFANIKIO YOYOTE YANA SABABU (38)

Na Pd. Dk. Faustin Kamugisha Mtandao chanya wa watu ni sababu ya mafanikio. Huwezi kupiga makofi kwa mkono mmoja. “Ukitaka kwenda kwa haraka sana, nenda peke yako. Ukitaka kwenda mbali, nenda pamoja na wengine.” (Methali ya Kiafrika). Hawa wanaotajwa kama ni wengine ni wale ambao wana mtazamo chanya. Ni wale ambao wanapiga makasia mtumbwi wako wa mafanikio ufike ufukweni. Ni ...

Read More »

Ujenzi wa barabara waathiri makazi Temeke

NA ALEX KAZENGA DAR ES SALAAM Wananchi wa Kata ya Makangarawe, Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam wameulalamikia ujenzi wa barabara za mitaa unaofanywa kwa kiwango cha lami katika mitaa hiyo wakidai kuharibu makazi yao. Ujenzi huo umeanza kutekelezwa hivi karibuni chini ya Mradi wa Uboreshaji wa Jiji la Dar es Salaam (DMDP), mradi huo unafanyika pasipo kuwahamisha wananchi ...

Read More »

Polisi yanasa bunduki 180, uhalifu wapungua

  KHALIF MWENYEHERI NA CATHERINE LUCAS, TUDARCO Jeshi la Polisi nchini limekamata silaha 187 katika kipindi cha Juni mwaka jana hadi Septemba mwaka huu, huku vitendo vya mauaji vikipungua kutoka 1,538 na kufikia 1,311 mwaka huu. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Jeshi la Polisi, silaha hizo zilizokamatwa katika maeneo mbalimbali nchini zilikuwa zikimilikiwa kinyume cha sheria na kutumika katika ...

Read More »

Maajabu ya viboko kisiwani Mafia

DAR ES SALAAM NA JUMA SALUM Kijiografia, Mafia ni kisiwa kilichoko Bahari ya Hindi, kilometa 120 kusini – mashariki mwa Jiji la Dar es Salaam na kilometa 20 mwambao wa pwani ya Wilaya ya Rufiji. Katika hali ya kushangaza, eneo la katikati la kisiwa hiki kidogo chenye ukubwa unaokadiriwa kuwa karibu nusu ya Kisiwa cha Unguja, wanapatikana wanyamapori aina ya ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons