Siasa

Ndugu Rais, amani kwanza mengine tutayapata kwa ziada

Ndugu Rais, lengo la maandiko yetu siku zote siyo kukosoa. Udhaifu wa kuandika kwa sababu unampenda mtu au unamchukia mtu, Mwenyezi Mungu katuepusha nao. Hatuandiki kwa ushabiki wa kumshabikia mtu au chama fulani. Wala hatuandiki hapa kwa lengo la kusifia au kupongeza. Tunaandika kile ambacho tunaamini kuwa ni ukweli mtupu, kwa lengo la kushauri tu. Tunaamini kuwa kwa hizi busara ...

Read More »

Uvunjaji Chako ni Chako wageuka kitanzi DODOMA

EDITHA MAJURA Imebuka sintofahamu kubwa kutokana na uvunjaji wa jengo la Chako ni Chako mjini Dodoma, baada ya kuwapo harufu ya eneo hilo kuviziwa na “wakubwa”, uchunguzi wa JAMHURI umebaini. Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma imevunja jengo lililokuwa maarufu kwa jina la Chako ni Chako, ambalo kwa miaka mingi limekuwa likitumiwa kwa biashara ya kuuza nyama ya kuku waliochomwa – ‘Kuku choma’. ...

Read More »

Pingu Yaibua `Zengwe’ kwa Mtuhumiwa wa Mauaji Moshi

Na Charles Ndagulla,Moshi Hatua ya kutofungwa pingu kwa mmoja wa Wakurugenzi wa Shule ya Sekondari ya Scolastica, Edward Shayo (63), anayetuhumiwa kwa mauaji ya aliyekuwa mwanafunzi wa shule hiyo, Humphrey Makundi imezua utata na kuhojiwa na baadhi ya mahabusu wa gereza la Karanga mjini Moshi. Shayo alikuwa miongoni mwa watuhumiwa 11 waliokamatwa kufuatia mauaji ya mwanafunzi huyo aliyetoweka shuleni hapo ...

Read More »

Msimamo wa AG Mpya Kuhusu Makinikia

Andiko hili ni la Mwanassheria Mkuu wa Serikali (AG), Dk. Adelardus Kilangi. Aliliandika mwaka jana akiwa Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine, Tawi la Arusha. Dk. Kilangi kitaaluma ni mwanasheria ambaye miongoni mwa maeneo aliyobobea ni kwenye sheria za madini. Aliandika makala hii ukiwa ni mtazamo wake binafsi akichangia kwenye mjadala wa makinikia baada ya kuwasilishwa kwa ripoti ya ...

Read More »

PROF ABDALLAH SAFFARI: Haja ya Kuwa na Mahakama ya Juu Tanzania

Tarehe 9 Desemba mpiga solo mahiri Tanzania kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Nguza Viking, kwa lakabu ya muziki, Big Sound alitoka Gereza la Ukonga, Dar es Salaam ambako alikuwa akitumikia kifungo cha maisha. Aliachiwa baada ya kunufaika na msamaha wa Rais John Magufuli alioutoa kwa baadhi ya wafungwa wapatao elfu nane katika hotuba aliyoitoa mjini Dodoma kusherekea siku ...

Read More »

Sumbawanga yanuka ufisadi

Vigogo wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga wamedaiwa kutengeneza vitabu bandia vya kukusanyia mapato ya ushuru na leseni za  uvuvi kwa wafanyabiashara wa samaki katika Ziwa Rukwa, JAMHURI inaripoti.  Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kwamba vitabu hivyo vimetengenezwa na baadhi ya wakuu wa idara ndani ya manispaa hiyo, kwa lengo kujiingizia mapato yanayokadiriwa kufikia zaidi ya Sh. milioni 100 ambazo ...

Read More »

Mzungu mchochezi anaswa Loliondo

Raia wa Sweden, Susanna Nordlund, anayetambuliwa kama mmoja wa wachochezi wakuu wa migogoro katika eneo la Loliondo, Ngorongoro mkoani Arusha, amekamatwa na kufukuzwa nchini. Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na Mkuu wa Wilaya (DC) ya Ngorongoro, Hashim Shaibu, ndiye aliyeongoza Kamati hiyo kwenda kumkamata. Sussana alikamatwa saa 2 usiku katika hoteli maarufu ya Onesmo iliyopo Wasso, akiwa anakula ...

Read More »

Manispaa Kinondoni ‘yauza’ barabara

Serikali Kuu na Manispaa ya Kinondoni wameruhusu ujenzi wa Shule ya Saint Florence Academy iliyopo Mikocheni “B”, Dar es Salaam juu ya barabara. Hatua hiyo, licha ya kuwa imevunja sheria za Mipango Miji, imekuwa kero na hatari kwa usalama wa wanafunzi na majirani wa kiwanja hicho namba 622. Pia imebainika kuwa mmiliki wa shule hiyo pamoja na familia yake, wanaishi ...

Read More »

Wazee ‘wamaliza kazi’ CCM

Baraza la Ushauri la Wazee wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), limeshatoa mapendekezo ya awali ya kumsaidia Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, ili kumpata mgombea urais atakayekiwakilisha chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, mwaka huu. Baraza hilo linaundwa na wenyeviti na makamu wenyeviti wastaafu. Wajumbe wake ni marais wastaafu – Ali Hassan Mwinyi (Mwenyekiti), Benjamin Mkapa, Dk. Salmin Amour, ...

Read More »

Yanayoendelea Afrika Kusini ni mwendelezo wa ubeberu

Hisia tupu hazitusaidii kuzikabili changamoto zenye uhalisia mwingi. Kiendeleacho Afrika Kusini ni matokeo ya muda mrefu wa kupandwa kwa saratani ya ubaguzi wa kijamii, kisiasa na kiuchumi.  Haiyumkiniki ni kile kitarajiwacho baada ya jamii na tawala kujisahau, wakatokea kudunisha baadhi ya watu na kusimika unyonyaji, dhuluma iliyotopea na kusakafia ubeberu kinyume cha thamani kuu ya utu.  Ninaamini bado wengi wa ...

Read More »

RC K’njaro amilikisha marehemu kiwanja

Ndugu zangu wanahabari, Januari 30 mwaka huu, niliwaiteni na kuwaeleza kwa kirefu kuhusu mgogoro wa kiwanja kilichokuwa na hati namba 10660 ambacho ndipo zilipo Ofisi za Kata ya Mawenzi ambacho zamani kilikuwa kikimilikiwa na The Registered Trustees of Mawenzi Sports Club kabla ya kutwaliwa na Serikali mwaka 2002. Lakini kama mtakavyokumbuka, niliwaeleza namna Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, ...

Read More »

Ugaidi Tanzania

Serikali imetakiwa iwe makini kuhakikisha inavitumia vyombo vyake vya ulinzi na usalama na wananchi kukabiliana na tishio la makundi ya kigaidi, hasa al-Shaabab kutoka Somalia. Mbunge wa Kigoma Kusini – NCCR-Mageuzi, David Kafulila ameliambia JAMHURI kwamba Tanzania inapaswa kuwa makini. Anasema suala la ugaidi linalozungumzwa kila mahali nchini linaweza kufanyika kutokana na magaidi kutekeleza uhalifu huo bila kujulikana kirahisi. Kwa ...

Read More »

‘Serikali imekurupuka, imeumbuka’

Serikali imeingia doa. Migomo wafanyabiashara na madereva wanaoendesha mabasi ya abiria, imetikisa nchi kiasi cha kufanya wadau kadhaa kueleza kuwa nchi imekosa sifa za uongozi. Tukio la kwanza, ambalo limekuwa likijirudia linahusu wafanyabiashara ambao mara kwa mara wamekuwa wakigoma kwa kufunga maduka kwa shinikizo la kuachiwa Mwenyekiti wao, Johnson Minja. Tukio la pili ni la madereva, ambao Ijumaa iliyopita walitekeleza ...

Read More »

Mahakama ya Kadhi fupa gumu bungeni

Kabla ya kuwasilishwa bungeni Aprili mosi, mwaka huu muswada wa Mahakama ya Kadhi, ulipata ugumu wa aina yake kwenye semina ya wa wabunge iliyolenga kuwaongezea ufahamu juu ya uanzishwaji wa mahakama hiyo.  Hata hivyo, kile kilichotokea kwenye semina hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma, ilitosha mamlaka husika kuondoa muswaada bungeni. Semina hiyo iliandaliwa na Wizara ya Katiba na ...

Read More »

Udini wapasua Bunge

*Tangazo la wabunge Waislamu kukutana lavuruga *Wakristo waandaa muswada wa Amri 10 za Mungu NA MWANDISHI WETU Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limekumbwa na mgawanyiko wa chini kwa chini wa udini.   Hali hiyo ilitojitokeza Alhamisi iliyopita ambako Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu, alitoa tangazo lenye kuashiria mgawanyiko wa kidini hasa wakati huu wa mjadala wa Mahakama ...

Read More »

Wenye VVU wakubali unyanyapaa kulinda CD4

Mbali ya kifungu cha 32 cha Sheria ya Kudhibiti Ukimwi namba 28/2008 kupiga marufuku unyanyapaa, watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU) wamesema tatizo hilo bado ni kubwa.   Kutokana na hali hiyo, jamii ya wenye VVU imedai imekuwa ikilazimika kukubaliana na unyanyapaa unaofanywa na baadhi ya watu ili kulinda CD4 zisipunguwe mwilini.   Walidai kuwa tangu janga hatari la ...

Read More »

Mama akodisha baunsa kumchapa mtoto wake

NA VICTOR BARIETY, GEITA Mtoto mwenye umri wa miaka 13 amelazimika kutoroka nyumbani na kwenda kuishi kwa wasamaria wema, baada ya kulemewa na kichapo kutoka kwa mwanaume mwenye kifua na misuli mipana (baunsa).  Mtoto huyo, mwanafunzi wa Darasa la Saba B, katika Shule ya Msingi Kalangalala, iliyoko wilayani hapa alikula kichapo na baunsa huyo aliyelipwa ujira Sh. 5,000 na mama ...

Read More »

Ngono: Diwani CCM matatani kugeuza mwanafunzi kimada

Diwani wa Kata ya Nyugwa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Donald Kabosolo, anafanya kazi ya ziada kuzima tuhuma dhidi yake juu ya uhusiano wa kingono na mwanafunzi wa sekondari ya kata hiyo iliyopo katika  Wilaya ya Nyang'hwale, mkoani Geita.

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons