Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Daniel Chongolo akiwasalimia akina mama waliofika kumpokea katika kata ya Masama Rundugai Chekimaji Hai mara baada ya kuwasili kukagua ujenzi wa kituo Cha Afya na nyumba za watumishi kijijini hapo Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.
Katika ujenzi wa Kituo hicho wananchi wamechangia jumla ya shilingi milioni 11 na Halmashauri ikichangia shilingi milioni 28 na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa shilingi Milioni 500
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Daniel Chongolo akivishwa mgolole kama ishara ya kumkaribisha Wilayani Hai alioowasili.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Daniel Chongolo akisalimiana na akina mama alipowasili kata ya Masama leo.

By Jamhuri