Wiki moja baada ya kuzinduliwa rasmi nchini, ORIJIN bado ni miongoni mwa bidhaa zinazozungumzwa na watu katika maeneo mbalimbali ya burudani. Kila siku kuna watu wanaoionja kwa mara ya kwanza, huku waliokwisha kuijaribu wakitoa maoni yao kuhusu ladha na uzoefu walioupata.
Miongoni mwa mambo yanayovutia wengi ni mchanganyiko wa ladha ya uchungu na utamu unaotokana na herbs, roots na fruits za Kiafrika.
Wapo wanaosema ladha hiyo imeleta hisia tofauti na walizozoea, huku wengine wakieleza kuwa imewakumbusha vinywaji vya asili walivyowahi kuvifahamu.
Kadri siku zinavyosonga mbele, maoni kutoka kwa watumiaji yanaendelea kuongezeka. Wengine wanaelezea uzoefu wao kupitia mazungumzo ya kila siku na wengine kwenye mitandao ya kijamii, jambo linaloifanya ORIJIN kuendelea kubaki kwenye mjadala.
Mbali na ladha yake, ORIJIN imeletwa katika aina tofauti ili kumpa mtumiaji uhuru wa kuchagua. ORIJIN Bitters inapatikana katika ukubwa wa mililita 750 na 200, huku ORIJIN Mixed (RTD) ikiwa chaguo jingine kwa wanaopendelea kinywaji kilicho tayari kwa matumizi.
Baada ya wiki moja tangu uzinduzi wake, ORIJIN inaendelea kujijengea nafasi kupitia maoni ya walaji wenyewe, hali inayodhihirisha kuwa gumzo kuhusu bidhaa hiyo bado halijafikia mwisho.


