Ligi dhaifu, Taifa Stars pia dhaifu!
Emmanuel Amunike! Alipata sifa sana wakati akiwa mchezaji lakini amejikuta akiwa garasa katika kazi ya ukocha. Sitaki kuzungumzia huko alikotoka, lakini ndani ya Taifa Stars ameshindwa kufikia malengo ya waajiri wake, nao wamemtoa kafara. Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, akaamua kuitisha mkutano, lakini ‘wababe’ wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)…