Zikiwa zimesalia siku chache michano ya kombe la Dunia ianze kutimua vumbi huko mashariki ya kati, unaweza ukawa unavuta picha michuano ya msimu huu itakuwaje!

Hivi ndivyo viwanja nane ambavyo michuano hiyo itachezewa hapo nchini Qatar kuanzia Novemba 20, 2022

1. Uwanja wa Al Bayt

Muonekano wa nje kwa juu uwanja wa Al Bayt

Uwanja huu upo jjini Al Khor ukiwa ni wa pili kwa ukubwa, unauwezo wa kubeba mashabiki 60,000 na hapa ndipo utakatwa utepe kwa mechi ya ufunguzi wa Kundi A kati ya Qatar dhidi ya Ecuador

Muonekano wa ndani uwanja wa Al Bayt

2. Uwanja Lusail Iconic

Muonekano wa nje uwanja wa Lusail Iconic

Uwanja huu upo jijini Lusail na ndio uwanja mkubwa zaidi ukiwa na uwezo wa kubeba mashabiki mpaka 80,000 na hapa ndipo Fainali za kombe zitafanyikia.

Mandhari ya ndani ya uwanja wa Lusail Iconic ukiwa na mashabiki

3. Uwanja Ahmad Bin Ali

Muonekano wa nje kwa juu uwanja wa Ahmad Bin Ali

Uwanja huu unauwezo wa kubeba idadi ya mashabiki wapatao 40,000 na upo mjini Umm Al Afaei

Mandhari ya ndani uwanja wa Ahmad Bin Ali

4. Uwanja AI Janoub

Muonekano wa nje uwanja wa Al Janoub

Uwanja huu una muonekano wa kipekee na umejengwa kwa ufundi wa aina yake ukiwa na uwezo wa kubeba mashabiki wapatao 40,000 na unapatikana katika jiji la Al Wakrah

Mandhari ya ndani ya uwanja wa Al Janoub

5.Uwanja Al Thumama

Muonekano wa nje uwanja wa Al Thumama

Uwanja huu wenye usanifu wa kipekee unaosadifu umbo la barghashia na utamaduni wa watu wa mashariki ya kati upo katika mji wa Al Thumama na una uwezo wa kubeba mashabiki 40,000 kwa mpigo.

Mandhari ya ndani ya uwanja wa Al Thumama

6. Uwanja Education City

Muonekano wa nje kwa juu uwanja wa Education City

Uwanja huu upo Al Rayyan na unauwezo wa kubebe mpaka mashabiki 40,000

Muonekano wa ndani ya uwanja wa Education City

7. Uwanja Khalifa International

Huu unabebe mashabiki 40,000 na unapatikana katika mji wa Aspire

Muonekano wa nje kwa juu uwanja wa Khalifa International

8. Uwanja 974

Muonekano wa uwanja wa 974 uliojengwa kwa makontena chakavu

Uwanja huu ni wa aina yake na umejengwa kwa makontena chakavu 974 ambayo namba hiyo pia ndiyo Code ya nchi ukiwa na uwezo wa kubeba mashabiki 40,000, uwanja huu unahamishika na huenda mashabiki wakawa wanafurahia upepo wa bahari kutokana uwanja huo kuwa mita chache kutoka usawa wa bahari mjini Ras Abu Aboud .

Madhari ya ndani ya Uwanja wa 974, uwanja huu unahamishika