Klabu ya Simba yamkana kocha aliyedakwa na dawa za kulevya

Uongozi wa Klabu ya Simba unaujulisha umma kuwa Muharami Said Mohammed maarufu Shilton hakuwa muajiriwa wa klabu yetu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na klabu hiyo leo Novemba 15,2022 imesema kuwa klabu hiyo ilimuomba na kukubaliana na Muharami kuwanoa makipa kwa muda kwa mwezi mmoja, wakati huo klabu ikiendelea kutafuta Kocha wa Magolikipa.Kwa mantiki hiyo klabu haihusiki na tuhuma zinazomkabili Kocha huyo.

Uongozi wa Simba unawaomba mashabiki wa klabu hiyo kuwa watulivu kwani hakuna athari yeyote kwa klabu kutokana na kadhia iliyomkumba Kocha huyo.

Hatua hiyo inafuata baada ya kocha huyo wa makipa kudawa pamoja na wenzake 9 kwa tuhuma za kukamtwa na dawa za kulevya aina Heloin yenye jumla ya Kilo 34.89.

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania (DCEA), Gerald Kusaya ametangaza watuhumiwa tisa wakiongozwa na Mmiliki wa Kambiaso Sports Academy, Alhaj Kambi Zubeir Seif pamoja na Kocha.