Timu ya wanawake ya Simba Queens imefanikiwa kuweka rekodi mpya katika soka la wanawake nchini kwa kutinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika Wanawake baada ya kuichapa timu Green Buffaloes Women ya Zambia, magoli 2 bila.

Timu ya Simba Queens imeandika historia kwenye soka la wanawake ngazi ya klabu nchini kwa kufanikiwa kuingia Nusu Faifali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya timu ya Green Buffaloes

Magoli ya Simba Queens yakifungwa na Asha Djafar dakika ya 64 na Opah Clement 78’

Mchezo wa Nusu Fainali Simba Queens itacheza dhidi ya AS FAR Club kutoka kundi A.