Na Meja Selemani Semunyu, Malawi

Rais wa Malawi Lazarus Chakwera ameishukuru Tanzania kupitia Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob Mkunda kwa ushirikiano inaouonyesha kwa nchi hiyo na jeshi lake kupitia michezo ikiwemo Gofu.

Rais Chakwera aliyazungumza hayo wakati wa sherehe za ufungaji wa mashindano ya gofu ya kuwaenzi na kuwachangia maveterani wa vita yaliyofanyika katika Uwanja wa Gofu wa Lilongwe nchini Malawi.

“Ninanawashuru Ndugu zetu kutoka Tanzania hakuna nchi ambayo haipati Changamoto za kiuchumi na hakuna Nchi ambayo haipambani kutatua shinda za wananchi wake na mahitaji yao lakini kikubwa ni kusaidiana na Kuchangiana kufanikisha hilo “ amesema Rais Nundwe.

wa Malawi Lazarus Chakwera (kulia ) Balozi wa Tanzania Malawi Mh Humphrey Polepole (Katikati ) na Mkuu wa Msafara wa Wachezaji kutoka Lugalo Gofu Meja Jenerali Ibrahim Mhona wakati wa kuzindua Mashindano ya Kuwaenzi Maveterani wa Vita jana (Ijumaa) Lilongwe Malawi (Picha na Meja Selemani Semunyu).

Kwa upande wake Mkuu wa Majeshi wa Malawi Jenerali Vicent Nundwe alisema ni heshma kubwa kwa jeshi lao kupata ugeni huo ambao umezidi kuongeza ushirikiano.

“ Najua mmesafiri kutoka Mbali kuja Malawi hii ni heshima kubwa kwetu tunawashukuru sana kwa kuacha shughuli zenu na kuja kutuunga mkono katika Mashindano haya.” amesema Jenerali Nundwe.

Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini Malawi Humphrey Polepole amesema kama ubalozi wanamshukuru Mkuu wa Majeshi Jenerali Jacob Mkunda kwa kuruhusu utekelezwaji wa Diplomasia kupita Michezo.

Naye Mkuu wa Msafara wa timu ya golf ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo Meja Jenerali Ibrahim Mhona alisema safari imekuwa na manufaa makubwa kwa Majeshi ya nchi zote mbili.

Aidha Mwenyekiti wa klabu ya Gofu ya Lugalo Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo alisema kwa Upande wa Klabu Baada ya Mashindano klabu sasa inajipanga kwa Mashindano ya Kombe la Mkuu wa Majeshi Mstaafu George Waitara.

Mbali na wachezaji wa Golf Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania liliwakilishwa pia na vikundi vya sanaa kutoka Mwenge ambavyo vilitumbuiza kwa pamoja na vikundi vya sanaa kutoka Malawi.

By Jamhuri