Moja kati ya heka heka katika  goli la Mbweni JKT wakati Mchezaji Gloria Benjamin wa Tamisemi Queens akijaribu kuwahadaa wachezaji  Zamzam Hamis (C), Jesca Ngisaise (GA) na Upendo Mpera (WA) huku mchezaji mwenzake Mersiana Samwel  (GD) akiwa tayari kutoa msaada katika mchezo mkali na wa kusisimua kati ya Tamisemi queens na Mbweni JKT uliomalizika kwa Tamisemi kushinda kwa magoli 52-37, katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Mchezaji Zamzam Hamis wa Mbweni JKT  akijaribu kuukamata mpira uliorushwa na Jesca Ngisaise (GA) wa JKT Mbweni  huku mchezaji Semeni Abeid (WA) naye akinyoosha mkono kuuwahi mpira huo katika mchezo wa Ligi ya Netiboli Tanzania uliochezwa jana mjini Morogoro ambapo Tamisemi ilishinda magoli 52-37
Mchezaji Lilian Jovin (GS) wa Tamisemi akifunga mojawapo ya magoli yaliyoipa ushindi timu yake dhidi ya JKT Mbweni katika mchezo mkali na wa kusisimua uliochezwa jana katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro ambapo Tamisemi ilishinda kwa magoli 52-37