JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: Maoni ya Mhariri

Umaarufu wa Rais uiunganishe Afrika

Ndoto ya miaka mingi ya viongozi waasisi wa Umoja wa Afrika (awali OAU na sasa AU) ya kuliona bara hili likishirikiana katika kila nyanja, si kwamba tu haijatimia, bali pia haionekani kutimia katika miaka 10 au 20 ijayo. Ukweli huu…

Miaka 26 baada ya ajali ya MV Bukoba…

Mwezi kama huu takriban miaka 26 iliyopita Tanzania ilikumbwa na msiba mkubwa wa kihistoria kuwahi kutokea baada ya meli ya abiria iliyokuwa ikitoka Bukoba, Kagera kuelekea Mwanza kupinduka na kuzama kwenye Ziwa Victoria. Ingawa hakuna idadi kamili iliyotolewa, lakini kwa…

Baada ya mshahara, sasa chapeni kazi

Wiki hii serikali imetangaza kukubali maombi ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) ya kupandisha kima cha chini cha mishahara kwa wafanyakazi wa umma nchini. Haya ni maombi ya muda mrefu na mara kwa mara serikali imekuwa ikishindwa kuyatekeleza…

Hatua zichukuliwe kulilinda Ziwa Victoria

Kwa zaidi ya wiki tatu sasa tumekuwa tukipokea malalamiko kutoka kwa wananchi wanaoishi pembeni mwa Ziwa Victoria, wakilalamika kuhusu kukithiri kwa uvuvi haramu. Malalamiko hayo ambayo kwa namna fulani tumeyathibitisha, yanatoka kwa raia wema waliopo mwambao wa ziwa hilo, hasa…

Pumzika Sheikh Abeid Amani Karume

Alhamisi hii Tanzania inafanya kumbukizi ya kifo cha Rais wa Kwanza wa Zanzibar, mwanamapinduzi Sheikh Abeid Amani Karume, ambaye sasa anatimiza miaka 50 tangu alipouawa kwa kupigwa risasi Aprili 12, 1972. Huo ndio uliokuwa msiba wa kwanza mzito kwa taifa…

Upandaji miti unahitaji wigo mpana zaidi

Miongoni mwa vichocheo vinavyoongeza tishio la ukame na mabadiliko ya tabia nchi linaloikumba dunia kwa muda mrefu sasa ni ukataji holela wa miti na uharibifu wa mazingira, hususan misitu. Ongezeko la ukataji miti ni tatizo kubwa kwa dunia na hata…