Uchumi

Tumekosea barabara za mwendo kasi (1)

Nianze hoja yangu kwa kumshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia uhai na amani ndani ya mioyo yetu, na hatimaye kuweza kuyafanya mengi tuyafanyayo kila kukicha likiwamo hili la ujenzi wa barabara za kuwezesha mabasi kwenda mwendo kasi. Kwa mantiki hiyo ni vema na haki na kila wakati kumshukuru Mwenyezi Mungu aliye mwingi wa rehema na mwenye kutujali muda wote wa ...

Read More »

Tunalindaje kampuni zetu?

Wakati fulani kule Marekani kulitokea malumbano makali baina ya kampuni mbili kubwa zenye nguvu na ushindani mkali. Kampuni zilizohusika katika sakata hili zilikuwa ni ile ya Brother na nyingine ni Smith Corona. Kampuni hizi zilijihusisha na utengenezaji wa bidhaa zinazofanana ikiwamo mashine za kudurufu (type writers), ‘keyboards’ za kompyuta, mashine za kusafisha hewa (air-conditioners) pamoja na vifaa lukuki vya kielektroniki. ...

Read More »

Tupo kwenye zama za ujasiriamali zilizoufukia ujamaa

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliamua kuanzisha mfumo wa kiuchumi wa Ujamaa na Kujitegemea miaka michache baada ya Tanganyika kujipatia uhuru wake.   Kwa kufanya hivyo alikuwa ameamua kufuata mawazo ya akina Adam Smith, David Ricardo, Milton Friedman, Fredrich Hayek, Ayn Rand Robert Owen, Pierre Leroux na Karl Marx kwa kuwataja kwa uchache; ambao wanatajwa kama waasisi na watetezi wa Ujamaa. ...

Read More »

Je, wote tuwe wajasiriamali?

Kwenye anga za uchumi na biashara kumekuwa na changamoto inayojirudia kutoka kwa baadhi ya wasomaji kuhusu dhana ya ujasiriamali.  Licha ya wasomaji kuzikubali makala hizi, lakini wamekuwa na walakini ikiwa inawezekana Watanzania wote tukawa wajasiriamali. Nafahamu kuwa si watu wote wenye ‘karama’ za kuwa wajasiriamali wa kibiashara. Hata hivyo, nimekuwa mwanaharakati wa kuhamasisha ujasiriamali wa kibiashara ili angalau Taifa lipate ...

Read More »

Uchaguzi 2015: Uchumi wetu unahitaji uongozi wenye mtazamo ya kitajiri

Nafahamu kuwa nchi iko kwenye joto la uchaguzi na joto hilo ni kubwa ndani ya chama tawala ikilinganishwa na ilivyo nje (kwenye vyama vingine). Wasomaji mnajua kuwa safu yangu ya uchumi na biashara huwa sizungumzii siasa hata tone. Hata leo sichambui siasa ndani ya makala hii; hivyo usiwe na shaka. Twende pamoja. Wasomaji wa muda watakumbuka kwamba mwaka huu nimeshapata ...

Read More »

CCM ina nia mbaya kwa makada wake?

Baada ya danadana ya muda mrefu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inayoendelea kukwamisha kumtangaza mgombea wao wa urais, sasa naamua kusema. Hii ni kwa sababu ni mwanachama wa kawaida na sina nafasi ndani ya vikao vya Kamati Kuu wala Halmashauri Kuu. Nimeona hivi kwa sababu hata ikitengenezwa mizengwe na majungu ya kila namna, bila ya kumsimamisha Edward Lowassa au Bernard ...

Read More »

Sababu nne za ushahidi wa kuambiwa haukubaliki kortini

Ushahidi wa kuambiwa ni nini? Ushahidi wa kuambiwa ni ule unaotolewa na mtu ambaye hakuona tukio likitendeka, hakusikia tukio likitendeka, hakuhisi wala kuonja, wala kunusa jambo lililo mbele ya Mahakama kama kosa isipokuwa aliambiwa na mtu mwingine aliyeona, kusikia, kuhisi, kunusa au kuonja. Hapa kuna watu wawili – kwanza aliyeona au kusikia na pili yule aliyeambiwa na huyu aliyeona au ...

Read More »

Nguvu ya mawazo katika mafanikio kiuchumi

Kila kitu kinachoonekana duniani kilianza na mawazo. Mawazo ndiyo kiwanda kikubwa cha uumbaji wote unaoonekana duniani. Hata katika vitabu vya dini tunaelezwa kuwa Mungu aliamua (Mawazo) kuumba mbingu na nchi. Ninaposoma Biblia kuhusu habari hizi za uumbaji wa Mungu, kuna kitu huwa najifunza kwa namna ambavyo Mungu aliumba mbingu na nchi. Kimsingi Mungu aliamua kuumba dunia hii pamoja na vyote ...

Read More »

Bandari Bagamoyo, kifo cha Bandari Dar

Imenichukua miaka miwili kufikiri juu ya hiki kinachoitwa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo. Ujenzi huu ulianza kutajwa mwaka 2010, na ilipofika Machi 2013, Rais wa China, Xi Jinping, akatia saini mkataba wa ujenzi wa bandari hiyo. Mkataba ukasema bayana kuwa ujenzi huu utatengewa dola bilioni 10. Nilisubiri kusikia Watanzania wanasema nini, ila muda wote naona kimya. Mkoa wa Mtwara kidogo ...

Read More »

Kumshitaki kwa jinai aliyevamia ardhi yako

Katika migogoro ya ardhi, yapo mambo mengi ambayo hujitokeza. Yumkini hii yote huwa ni katika kusaka haki.  Liko jambo moja ambalo ni muhimu watu kulijua hasa wale ambao tayari wamejikuta katika migogoro ya ardhi.  Mara nyingi imekuwa ikitokea pale mtu fulani ana mgogoro wa ardhi na mtu mwingine kumwendea polisi na kumshitaki kwa jinai ya kuvamia ardhi yake (criminal trespass). ...

Read More »

Wafanyakazi ndiyo injini katika ujasiriamali

Mwishoni mwa Februari mwaka huu nilikuwa nikisafiri kutoka Wilaya ya Mvomero kuelekea Kilombero mkoani Morogoro. Nilipofika Morogoro mjini niliingia kwenye basi moja ambalo linafanya safari zake kati ya Morogoro mjini na Ifakara.  Muda niliokata tiketi katika basi hilo ilikuwa ni saa tisa na nusu jioni, lakini ndani ya hilo basi nilikutana na abiria ambao walikata tiketi majira ya saa tatu ...

Read More »

Magari mengi nchini ni utajiri au ulofa?

Kwa muda mrefu sasa nina dukuduku la kuuliza Wanatanzania wenzangu hasa wale wachumi waliobobea kama akina Profesa Ibrahim Lipumba au Profesa Simon Mbilinyi vile.   Suali langu; ni vigezo gani katika Taifa linaloendelea vinaonesha kukua kwa uchumi katika Taifa?   Wako wachumi wengi hapa nchini lakini hapa nimewataja hawa maprofesa wawili kwa vile kila mmoja kwa muda fulani aliwahi kuwa ...

Read More »

Ni vema kudhibiti nguvu ya fedha

Kimsingi fedha inapomjia mtu huwa inaambatana na nguvu fulani kubwa sana yenye chembe chembe za umiliki. Ni vema tukafahamu kuwa duniani kuna nguvu nyingi sana, lakini nguvu ya fedha pamoja na nguvu ya mamlaka zinatawala nguvu nyingine kwa sehemu kubwa. Nguvu ya fedha na nguvu ya mamlaka zinaingiliana na kutegemeana ijapokuwa kuna sehemu zinaachana. Mathalani, mtu anaweza kuwa na mamlaka ...

Read More »

Amani Tanzania inatuponyoka taratibu

              Kwa muda sasa nimefuatilia matukio yanayoendelea nchini. Nimesoma habari mbalimbali zinazoonesha askari polisi wakiuawa kwa risasi na kunyang’anywa bunduki katika maeneo kadhaa hapa nchini. Tumesikia ‘magaidi’ katika mapango ya Amboni Tanga.  Vituo vya polisi vimetekwa. Tumeshuhudia wafanyabiashara wakigoma na kuipa amri Serikali. Nikumbushie kidogo tu kuwa mwezi uliopita, Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Ndogondogo, Joseph ...

Read More »

Mimi ni Mwalimu, niliingia siasa kama ajali tu

                  Watanzania mwaka huu wanaingia kwenye Uchaguzi Mkuu wa tatu, bila ya mwasisi wa Taifa hili, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Taarifa zinasema kwamba Nyerere alizaliwa mwezi kama huu, tarahe 13 (ya jana), mwaka 1922 na kwamba kama angelikuwa hai, jana angesherehekea miaka 93 tangu kuzaliwa kwake. Tutafakari. Historia inatueleza kuhusu mambo mbalimbali ...

Read More »

Matabaka katika elimu yanarudi?

Siku za karibuni hapa Dar es Salaam, jiji letu kioo cha Taifa hili, kumeonekana mabasi kadhaa yaliyoandikwa “INDIAN SCHOOL BUS” na mengine “YEMEN SCHOOL BUS”.  Baadhi yetu walimu wa zamani tumeshtuka na kufikiria mbali kule tulikotoka enzi za ukoloni. Bado tukawa na maswali zipo kweli shule za mataifa hayo?   Tukaja kugundua kumbe kweli hapa Dar es Salaam kuna shule ...

Read More »

Barua ya kijasiliamali kwa wanawake

Ndugu akina mama na akina dada, nawasalimu kwa salamu za fedha ziletwazo na uchumi na ujasiriamali. Naamini barua hii itawafikia salama mkiwa mmesherehekea Pasaka kwa amani na mkiwa mmeanza robo ya pili ya mwaka kwa mafanikio.  Si mara yangu ya kwanza kusema na wanawake kuhusu ujasiriamali, lakini ni mara yangu ya kwanza kuwaandikia barua maalumu. Nimeamua kuwaandikia kwa sababu ninawaamini ...

Read More »

Mikopo ni sehemu ya biashara

  Visa na mikasa ya wajasiriamali kukopa na baadaye kujikuta wakishindwa kurejesha mikopo yao ni vingi sana mahali pote, si tu Tanzania bali duniani kote. Mikopo imekuwa chanzo cha baadhi ya wajasiriamali na wafanyabiashara kudhalilika, kurudi nyuma kimaendeleo na hata kukimbia maeneo yao. Hata hivyo, huo ni upande mmoja wa mikopo na tena ulio mdogo sana; upo upande wa pili ...

Read More »

Kukataa rushwa ni ukombozi kwetu

Na Angalieni Mpendu   Rushwa ni adui wa haki, sitapokea wala kutoa rushwa. Msemo wa ilani hii umesemwa miaka mingi katika nchi yetu, tangu awamu ya kwanza hadi hii ya nne ya utawala wetu huru wa Watanzania.   Nasema kabla nchi yetu kuwa huru, enzi ya ukoloni rushwa ilikuwapo, lakini ilikataliwa na kuogopwa mithili ya mnyama simba msituni anavyoogopwa na ...

Read More »

Wateja wa ulimwengu mpya wa biashara

Katika makala mbili zilizopita nilikuwa nikichambua kuhusaina na ulimwengu mpya wa biashara. Nilieleza kwa kina namna uchumi ulivyohama kutoka viwanda kwenda taarifa na huduma, na hivyo kuathiri namna biashara zinavyofanyika. Katika makala zile mbili nilieleza kwa sehemu kubwa kuhusu taarifa zinavyoathiri mienendo ya biashara. Katika makala hii leo ninamalizia kwa kuangalia uchumi wa huduma lakini mahususi tunaangalia kizazi cha wateja ...

Read More »

Watoto wa marehemu (mke/mme) hugawanaje mirathi?

Mara nyingi nimeandika kuhusu mirathi, lakini zaidi nimegusia habari ya usimamizi wa mirathi. Leo nimeona ni muhimu kueleza mgawo wa mirathi kwa kuangalia nani anapata nini kupitia sheria ya mirathi ya Serikali. Mgawo ukoje ikiwa mume amefariki? Kama mume amefariki na akaacha mjane na watoto, basi moja ya tatu (1/3) ya mali za marehemu zilizo kwenye mirathi anatakiwa apewe mke ...

Read More »

Nini ufanye ukihisi mwenza wako anataka kuuza nyumba, kiwanja?

Upo wakati katika ndoa ambako mmojawapo anaweza akawa anataka kuuza au kubadili jina la nyumba/kiwanja bila ridhaa ya mwenzake ilhali nyumba hiyo ni ya familia. Lakini pia nje ya hilo, kuna mazingira ambayo mtu anaweza kuwa si mwanandoa, lakini ana maslahi katika nyumba au kiwanja cha mtu fulani na anataka kuzuia nyumba/kiwanja hicho kisibadilishwe jina au kisiuzwe.   Kisheria jambo ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons