Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Manendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC mjini Moshi akiendelea kupatiwa matibabu baada ya kufikishwa hospitalini hapo jana usiku alipougua ghafla.

Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai na kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni (KUB), alifikishwa katika hospitali hiyo jana saa mbili usiku. Baada ya kufukishwa, madaktari walimwekea mashine ya kumsaidia kupumua baada ya kuonekana hakuwa kwenye hali nzuri.

Basil Lema ambaye ni Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Kilimanjaro alithibitisha kiongozi huyo kulazwa KCMC na kueleza kwamba, aliugua ghafla na walipompeleka KCMC, madaktari walilazimika kumwekea oksijeni ili kuimarisha afya yakelakini baadaye waliondoa hiyo oksijeni baada ya afya yake kuimarika.

Taarifa kuhusu ugonjwa unaomsumbua kiongozi huyo wa chama kikuu cha upinzani nchini hazijawekwa wazi.

2543 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!