MOTO umewaka na kuteketeza gari dogo aina ya Toyota Ractics, leo Jumatatu, Julai 2, 2018 katika Daraja la Nyerere (Kigamboni) jijini Dar es Salaam huku mwenye gari akifanikiwa kutoka nje ya gari na kukimbilia sehem salama.

Chanzo cha ajali hiyo imedaiwa kuwa ni hitilafu ya umeme wa gari hiyo pindi limefika kwenye kukata ticket hitilafu hiyo imetoka na kuanza kuungua, juhudi za kuliokua gari hilo zilifanyika na kufanikiwa kuuzima moto huo hali likiwa limeshaungua mbele.

Inadaiwa ajali hiyo imetokea wakati dereva wa gari hilo akilipia fedha ili avuke ng’ambo, lakini pia huku kukiwa hakuna taarifa ya majeruhi wala vifo vilivyoripotiwa kutokana na ajali hiyo.

2062 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!