Kim Jong-un amekuwa kiongozi wa kwanza kutoka Korea kaskazini kuingi Korea kusini tangu kumalizika kwa vita vya Korea mwaka 1953 na kuandika historia mpya baina ya mataifa hayo mawili.

Kim katika mkutano huo aliandamana na maafisa tisa , ikiwemo dadake ambaye aliongoza ujumbe wa Korea Kaskazini katika michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi nchini Korea Kusini mapema mwaka huu.

Hatua hiyo iliyoshangiliwa kwa mbwembwe za kila aina kiongozi wa huyo wa Korea Kusini na mwenzake wa Korea Kaskazini walisalimiana kwa mikono wakiwa  mpakani  mwa nchi hizo na kufufua matumaini mapya.

Vyombo vya habari vya Korea kazkazini na kusini  viliwasifia viongozi hao  Kim Jong Un na mwenzake  Moon Jae-in kwa kufanikisha mkutano huo wa kihistoria kwa namna nyingi huku  wakifikia makubaliano ya kufanya kazi kwa pamoja.

Wadadisi wa maswala ya kisiasa wanasema si rahisi kutabiri azma ya baadaye ya Kim Jong Un hasa  iwapo kweli atatupilia mbali miradi yake ya kinyuklia, wakihoji kuwa hakutoa hakikisho lolote linaloweza kuaminika.

Rais wa Marekani Donald Trump akizungumzia mkutano huo amesema Marekani itaendelea  kuishinikiza Korea kaskazini kuachana na miradi yake ya kinyuklia licha ya mafanikio makubwa ya mkutano miongoni mwa viongozi hao.

Rais Trump pia amesisitiza nia  yake ya kukutana na kiongozi huyo wa Korea kaskazini kwa matumaini kwamba ataweza kumshawishi asiendelee kujilimbikizia silaha hizo hatari zinazopingwa duniani.

Lengo la mazungumzo

Lengo kuu la mazungumzo kati ya viongozi hao ilikuwa ni kuzungunmzia mpango wa kinyuklia wa Korea Kaskazini  hata hivyo Seoul imeonya kwamba kuishawishi Pyongyang kuwacha mpango wake wa kinyuklia itakuwa vigumu .

Mkutano wa viongozi hao ulikuwa  ni wa tatu kufuatia mikutano mingine iliofanyika 2000 na 2007 umeongeza kufufua matumaini ya uwezekano wa kumalizika kwa mgogoro uliodumu kwa miaka mingi.

By Jamhuri