Gharama za maisha zinatuelemea

Tanzania tunakwenda wapi jamani, gharama za maisha zinapanda na kuongezeka kila kukicha, sasa tumeanza kutozwa kodi ya kulipia laini za simu za mkononi! Enyi viongozi tuliowapa dhamana tutazameni Watanzania kwa jicho la huruma.

Aziz Msafiri, Dodoma

0757 100079

Namuunga mkono Dk. Salim

Kauli ya Dk. Salim Ahmed Salim ya kukerwa na matamshi ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, haiwezi kupita bila kuungwa mkono na Watanzania nikiwamo mimi. Kauli hiyo ‘wapigwe tu’ inakwaza usalama na utengamano wa kitaifa. Viongozi wastaafu wengine mko wapi?

Charles H. Kagonji

0784 200136

 

Serikali isiwanyanyase wamachinga

Serikali iache kuwanyanyasa, kuwafukuza na kuwapora wamachinga bidhaa zao kwani hilo haliwezi kuwa mwisho wa uchafu katika Jiji la Dar es Salaam. Suluhisho la uchafu jijini ni kuboresha miundombinu.

Mpenda amani Tanzania

0715 577991

 

Hosipitali ya Nzega imulikwe

Wauguzi na wafanyakazi wengi wa Hospitali ya Wilaya ya Nzega hawafanyi kazi ipasavyo, wao wamejikita zaidi katika kuhudhuria semina nyingi, lakini pia kuna upendeleo mkubwa katika kuteua majina ya wafanyakazi wa kuhudhuria semina.

Mazigo B, Nzega

0755 287163

 

Sitta vipi kuhusu Dowans?

Waziri Samwel Sitta asimame sasa aseme kuhusu Dowans. Mbona yuko kimya? Mbona yeye [Sitta] na Dk. Harrison Mwakyembe hawajazungumzia kitendo cha Rais wa Marekani, Barack Obama kutembelea mitambo ya Symbion?

0756 984106


Smart Partnership Dialogue

Serikali iwaeleze wananchi kinagaubaga faida za mkutano wa Smart Partnership Dialogue, vinginevyo tutaamini kwamba kuna chembe ya ufisadi katika matumizi ya Sh bilioni nane kugharimia mkutano huo.

0756 984106

 

Vyama vya siasa viangaliwe

Vyama vya siasa viangaliliwe, vinakaanga mbuyu vinaachia wengine watafune, wao viongozi hawakamatwi. Wananchi wanabururwa na vyama wamefunikwa na vitambaa machoni?

0782 181110

 

Milipuko mabomu mtego wa panya?

Milipuko ya mabomu Arusha, mliosema kuwa nchi haitawaliki mnachekelea kichaka kinachoungua mithili ya mtoto wa nyani ilhali kichaka maskani yenu! Kubali usikubali, mtego wa panya kuna wakati hata mtegaji hudhuriwa na mtego huohuo.

Mwl. Nyemenohi, Singida

0782 556681

1084 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!