Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma imeiharisha kesi inayomuhusu aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM na Mbunge wa Donge, Zanzibar Sadifa Juma Khamis anayetuhumiwa kwa rushwa.

Sadifa Juma Khamis alikamatwa nyumbani kwake Dodoma December 9, 2017 kwa tuhuma za Rushwa akidaiwa kuwapa wajumbe kutoka Kagera vinywaji na pia kuahidi kuwalipia nauli ili wamchague kuwa kutetea tena kiti chake cha Mwenyekiti mpya wa UVCCM taifa.

Decemba 19 mwaka huu mahakama hiyo ilikubali kumuachia kwa dhamana Mbunge huyo na kuiahirisha kesi hiyo mpaka leo January 18 ambapo pia imeshindwa kuisikiliza.

Mahakama hiyo ilimpatia dhamana Sadifa baada ya kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wenye bond ya shilingi milioni moja kila mmoja.

2254 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!