Mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru, amerejeshwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kuendelea na matibabu.
Mzee Kingunge aliruhusiwa kutoka hospitalini hapo Januari 10 ili kwenda kushiriki mazishi ya mkewe, Peras Ngombare Mwiru yaliyofanyika Alhamisi katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salam.
Mtoto wa kiume wake wa kiume, Kinjekitile Ngombare Mwiru, amekaririwa na gazeti moja la kila siku, akisema, baada ya baba yake kumzika mkewe amerejea hospitalini katika chumba cha wagonjwa mahututi, ICU, ili kuendelea na matibabu kama alivyotakiwa na madaktari wake.
Mzee Kingunge alilazwa hospitalini hapo baada ya kushambuliwa na mbwa nyumbani kwake eneo la Victoria jijini Dar es salam hivi karibuni.

1865 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!