Simon JackUtafiti umeonesha kuwa wanaume wenye umri kati ya 40-50 wamo katika hatari kubwa ya kujinyonga ikilinganishwa na wanawake.
  Kijana mmoja kutoka England, Simon Jack, amefanya utafiti huo baada ya baba yake kujiua katika siku yake ya kuzaliwa miaka 25 iliyopita akiwa na umri wa miaka 44.
Jack anasema alianza kuwa mdadisi kwa simulizi zote au habari kuhusu watu wanaojiua na amegundua kuwa wote ni wanaume.


“Sikujua kuwa kujiua ni adui mkubwa wa watu wenye umri chini ya miaka 50, ila sasa nafahamu kwanini wanaume mia moja wamejiua ndani ya wiki,” anasema, akitaja takwimu hizo za Ulaya.
Idadi hiyo imekuwa kubwa zaidi kuliko wakati wowote katika miaka 14 iliyopita, ya wanaume wanaomaliza maisha yao wenyewe ni mara nne ya wanawake.


Jack alitamani kufahamu sababu inayowafanya wanaume kufanya matukio hayo zaidi na kama kuna namna yoyote ya kuzuia mauaji haya: “Nilijiuliza nini kinachosababisha wanaume hawa kufanya hivi?
“Miaka 40 ni miaka ambayo mtu ana majukumu mengi, unaweza kudhani kuwa mke wake amemuacha na kuchukua watoto wote, au kapoteza kazi yake katika umri huo wakati ni vigumu kupata nyingine…
“…Au sababu yoyote ambayo inaweza kumpa shinikizo mwanaume ambaye anahitajika kuhudumia familia yake?’’


Kwa upande wa baba yake Jack, haikuwa hivyo kwani alikuwa ni baba mzuri mwenye upendo kwa familia yake, mwenye uwezo na umaarufu.
Kila mtu atakubali kuwa ni tatizo kubwa katika familia pale unapompoteza mtu kwa sababu ya ugumu wa maisha uliokithiri au kuachwa na mpendwa wako.


Wengine walitoa maoni kuwa wengi wanaojiua ni ushahidi tosha kuwa wana matatizo ya kiakili au wana msongo wa mawazo au huzuni katika maisha.
Profesa Rory O’Connor, anayeongoza kituo maarufu duniani cha utafiti katika Chuo Kikuu cha Glasgow, anasema tabia ya kujiua ni tatizo la kisaikolojia ambalo hutokana na upungufu wa kiakili.


Ingawa watu wenye matatizo ya akili huwa ni vigumu sana kujiua. Tafiti zinasema ni asilimia tano tu ndiyo wanaoweza kujiua kutokana na upungufu wa akili.
Hata hivyo, katika uamuzi kuna tofauti kubwa kati ya namna wanaume na wanawake wanavyoweza kujielezea matatizo yao na kuyatatua.


“Wanawake huwa wanatumia njia za kujieleza ambazo ni rahisi watu kumuokoa tofauti na wanaume,” anasema Jack.
Jack anasema, “Natamani kujua nini kilimpata baba yangu kwani fumbo hili linaweza kujibu maswali ya familia nyingi wenye matatizo kama yangu.”
 
Makala hii imetafsiriwa kutoka mtandao wa uhusiano wa BBC.

3046 Total Views 2 Views Today
||||| 1 I Like It! |||||
Sambaza!