Msanii  maarufu  wa muziki wa Pop, Lady Gaga, anatarajiwa kutumbuiza katika tuzo za muziki za MTV zitakazofanyika Agosti, mwaka huu. Litakuwa onesho lake la kwanza baada ya kufanyiwa upasuaji wa sehemu za nyonga.

Katika onesho hilo, Lady Gaga (27) ambaye ni mshindi wa tuzo za Grammy anatarajia kutoa wimbo wake mpya ulioko kwenye albamu yake ya ‘ARTPOP’ anayotarajia kuizindua mapema mwezi Novemba, mwaka huu.

 

Lady Gaga ni mmoja wa wasanii ambao wamekuwa na mwonekano tofauati wanapokuwa jukwaani kutokana na mtindo wa mavazi yao ambayo huwaacha watazamaji midomo wazi. Moja ya mavazi yake yaliyopata kutamba nayo ni pamoja na lile lililotengenezwa kitambaa mithili ya nyama mbichi.

 

 

1120 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!