Katika toleo lililopita tuliishia katika aya isemayo: “Ngoja nimtumie barua pepe, ninaona hapatikani,’’ alisema yule mhariri wa makala alizokuwa akituma Noel. Walikuwa hawajawahi kuonana hata siku moja na Noel, Noel alikuwa hajawahi kufika katika ofisi za gazeti hilo. “Fanya mawasiliano naye, makala zake ninazipenda, zimepangika na anachambua vema,’’ aliongeza mhariri mkuu. Sura ya Noel waliijua kupitia picha aliyokuwa akiambatanisha katika makala zake. Sasa endelea…

Baada ya mhariri kumzungumzia Noel ikawa wasaa wa wengine kuanza kuulizana: “Kwani huyo kijana anaishi wapi?’’ aliuliza dada mmoja ambaye alikuwa akisoma makala za Noel. Yule Mhariri wa makala za Noel akamwambia alikuwa akiishi nje ya jiji hilo. Wakawa na hamasa na shauku ya kutaka kuonana na Noel ili kumfahamu vema.  

“Ila huyu kijana anaandika vizuri sana,’’ alisema mhariri mwingine wa makala za uchunguzi.

Vijana waliokuwa mtaani kwao Noel walikuwa wamekaa katika moja ya vijiwe vyao wakizungumza mambo yao. “Mbona siku hizi simsikii Noel?’’ aliuliza kijana huyo ambaye alikuwa akimkatisha tamaa Noel kipindi alipoanza kuandika makala kwenye gazeti.

Vijana waliokuwa mtaani kwao Noel walikuwa wamekaa katika moja ya vijiwe vyao wakizungumza mambo yao. “Mbona siku hizi simsikii Noel?’’ aliuliza kijana ambaye alikuwa akimkatisha tamaa Noel kipindi alipoanza kuandika makala kwenye gazeti. 

“Hawezi yule, ametangaza sasa ameingia kwenye magazeti, huko nako atashindwa tu,’’ alisema kijana mwingine ambaye naye alikuwa akimtamkia Noel maneno hasi. “Sijui siku hizi yuko wapi?’’ aliuliza mwingine. 

Noel alikuwa na mawazo tofauti na ya vijana wenzake pale mtaani. Kilichokuwa kikifanya Noel kuongelewa vibaya  na vijana wenzake ni kutokana na yeye kuwa mbali na tofauti na wao, lakini pia kuwa na mawazo yaliyokuwa hayaendani na wao. 

Yeye alitamani kufanya uandishi, lakini wenzake walikuwa hawana mawazo hayo. Wao walikuwa na mawazo ya anasa na vitu vingine vyenye shabaha hasi katika maisha yao. 

Mama yake Noel alikuwa akipita kuelekea kwa mchungaji, kwa kuwa siku hiyo alikuwa na ahadi ya kukutana na mchungaji. Akasikia yote yaliyokuwa yakiongelewa kuhusu Noel, akatikisa kichwa chake na kushangaa.

“Hawa wanamsema Noel mwanangu!’’ Ilimuumiza, kwa kuwa hawakumuongelea vizuri, bali walimuongelea kwa namna mbaya. Maongezi ya vijana wale yaliendelea: “Hana lolote Noel; kwanza, kwao umaskini umetawala,’’ alisema kijana ambaye alikua na kucheza pamoja na Noel. 

Lakini tabia ya Noel kubezwa haikuishia hapo. Noel alikuwa miongoni mwa vijana waliokuwa wakihudumu kwenye madhabahu ya kanisani. Alikuwa akipenda sana kufanya kazi ya Mungu. Hata hivyo wahudumu wenzake pia walikuwa wakimbeza na kumuita majina yasiyofaa. Jina alilokuwa amepewa Noel na wahudumu wenzake lilikuwa ni ‘bata mchafu’.

Wakati vijana hao wa mtaani kwao Noel walipokuwa wakimzungumzia, mama yake alikuwa amekaa pembeni akiwasikiliza. Mara akapita mmoja wa wahudumu waliokuwa wakitumikia kanisani pamoja na Noel. Alikuwa katika matembezi yake, vijana wakamuona na kumuita: “Emmanuel!’’ Aliita mmoja wa vijana waliokuwa wamekaa katika kile kijiwe cha vijana wa mtaani kwao Noel.

“Naam!’’ aliitika Emmanuel ambaye alikuwa mnafiki na muongo, mtu mwenye kupenda kuongelea maisha ya wengine.  

“Za siku, Noel bado anatumikia kanisani?’’ aliuliza mmoja wa vijana wale wa kijiweni. Emmanuel akamjibu: “Aliacha siku nyingi sana, yaani yule habadilishi nguo zake. Alikuwa anavaa suruali hiyo hiyo moja.’’ Wakati Emmanueli akizungumza hayo, Mama Noel alikuwa amesimama jirani, na alipomtazama alimkumbuka, kwa sababu kuna siku alifika na Noel nyumbani na wakala chakula pamoja.

“Kumbe huyu naye ni wa ovyo, anamsema Noel vibaya namna hii!’’ alijisemea moyoni Mama Noel. Akaamua kupita katikati ya vijana wale walipokuwa wamekaa. Baada ya Mama Noel kupita, vijana wale wakakaa kimya pasipo kuongea chochote. Mama Noel ingawa alichukia, aliamini mambo kama hayo huwa ni sehemu ya maisha, akapuuza na kuendelea na safari yake.

***

Ulikuwa ni muda wa saa kumi jioni Meninda akiwa hajaridhika na kile alichokuwa ameambiwa na yule mtu aliyekuwa akihusika na jarida lao. Akaamua kwenda katika ngazi ya juu zaidi, akaingia ofisini kwa mkurugenzi aliyekuwa akihusika na machapisho yote, vikiwemo vitabu pamoja na vitu mbalimbali vilivyohusiana na wakimbizi. Meninda akaingia na kufanikiwa kumkuta mkurugenzi akiwemo ofisini.

“Meninda karibu,’’ alisema mkurugenzi huku akisimama na kusalimiana na Meninda.  “Asante, hatuonani?’’ alisema Meninda akiwa anatabasamu. “Tunapishana, muda mwingine ninakuwa nimo safarini,’’ alisema mkurugenzi. 

Meninda hakutaka kupoteza muda wake, alianza kumwelezea kile kilichompeleka pale. 

“Nina kijana nyumbani ana uwezo mzuri wa uandishi wa vitabu, kwanini msimpe nafasi?’’ alisema Meninda. Mkurugenzi alifikiria kwa dakika chache kisha akamjibu:

68 Total Views 4 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!