Malcom akamilisha uhamisho wa £36.5m kutoka Bordeaux kuelekea Barcelona

Winga wa Brazil Malcom amekamilisha uhamisho wa kitita cha £36.5m kwa kujiunga na Barcelona kutoka Bordeaux.

Mkataba huo ulitangazwa mara ya kwanza siku ya Jumanne baada ya mabingwa hao wa Uhispania kuwashinda Roma katika kupata saini ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21.

“Hii ni ndoto ya utotoni ambayo imetimia”, alisema Malcom, ambaye bado hajaichezea timu ya taifa ya Brazil .”Natamani kuanza kucheza”.

Roma inafikiria iwapo ina kesi ya kuwasilisha baada ya kuafikiana na Bordeaux siku ya Jumatatu, wakisubiri vipimo vya kimatibabu kufanywa.

”Najua ni changaomoto kuichezea Barcelona , lakini hii ni ndoto niliokuwa nayo tangu nikiwa mdogo”, alisema katika hafla ya vyombo vya habari ilioandaliwa na Barcelona inayoelekea Marekani.

Barcelona italazimika kulipa dau la awali la Yuro 41m huku kitita chengine cha Yuro 1m tofauti kikitolewa.

Malcolm aliyefunga magoli 20 na kuandaa mengine 13 katika mechi 84 za Bordeaux atajiunga na Barcelona katika ziara hiyo ya Marekani.

Ni mchezaji wa pili wa Brazil kusajiliwa na klabu hiyo msimu huu baada kiungo wa kati Arthur kujiunga kutoka Gremio kwa dau la £35.5m.

Barcelona pia imemsajili beki wa kati wa Sevilla Clement Lenglet kwa kitita cha Yuro milioni 35.9 (£32m).

Mkurugenzi wa michezo katika klabu ya Roma Monchi alisema kuwa Malcom, ambaye pia alikuwa amehusishwa na uhamisho wa kuelekea katika ligi ya Premia huku Arsenal, Everton na Tottenham wakiwa na hamu.

Tayari ya stakhabadhi zilikuwa zimetolewa kati ya Roma na Bordeaux kabla ya klabu hiyo ya Itali kulazimishwa kuongeza dau walilotoa kufuatia hatua ya Barcelona kutoa kitita cha juu.

Lakini Roma ilitaka kuwasilisha ombi jingine huku Monchi akiambia mtandao wa Roma siku ya Jumatatu : Nilishangaa kuambiwa kwamba maajenti na Bordeaux walitaka tutoe dau jingine la kiwango cha juu huku Barcelona wakiendelea kutaka kuweka makubaliano na mchezaji huyo. Niliwaambia imetosha kwa kuwa hatukuwa tayari kuingia katika mnada.

2742 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!
Tags :
Show Buttons
Hide Buttons