Mwanariadha wa Kenyan Conseslus Kipruto alikaidi pigo la kupoiteza kiatu mapema ili kuibuka mshindi wa mbio za mita 3000 kuruka viunzi na maji katika ligi ya almasi ya IAAF Diamond League mjini Zurich, nchini Switzerland.

Baada ya kupiga kona moja ya uwanja kiatu chake cha kushoto kilitoka lakini hilo halikumzuia .

” Ilikuwa kisirani .Lakini nilipata motisha ya kupigana zaidi ili niendelee vyema”, alisema baadaye.

Kipruto ndio bingwa wa Olimpiki na na wadunia katika mbio za kuruka viunzi na maji. Alimpita Soufiane El Bakkali katika mita za mwisho baada ya kuruka kiunzi cha mwisho akiwa wa pili.

”Nimepata jeraha kwa sababu nilipoteza kiatu changu, alisema baada ya kukamilisha mbio hizo”.

Baadaye alituma ujumbe wa twitter:

Ilikuwa vigumu na uchungu kukimbia bila viatu, lakini nilikuwa na moyo wa ujasiri ya kutokubali kushindwa , mashabiki walikuwa wazuri na nikaamua kuendelea ili kushinda.

Baada ya mbio hizo mwanariadha huyo wa Kenya aliguchia na kuondoka katika uwanja akiwapungia mkono mashabiki.

Wakenya katika mitandao ya kijamii ikiwemo naibu rais William Ruto wamekuwa wakimpongeza Kipruto kwa ushindi huo

Please follow and like us:
Pin Share