MAMA mzazi wa Mwanamitindo maarufu Bongo Hamisa Mobeto, Shufaa Lutigunga amefunguka kuwa hayuko tayari kuolewa na “Serengeti Boy” wakati watu wazima wenzie wapo, kitendo ambacho kimetafsiriwa kuwa ni kumchana mama Esma aliyeolewa hivi karibuni na kijana mwenye umri mdogo kulinganisha na yeye.

Mama Mobeto alisema kuwa, sasa hivi ameshakuwa mtu mzima na ni bibi mwenye wajukuu hivyo kuolewa na kijana mdogo ni kujishushia hadhi kama mama na bibi pia.

“Jamani mimi kama ni kuolewa basi nitaolewa na mtu mzima mwenzangu kwasababu Serengeti Boy kwangu haiwezekani, nahitaji kuolewa kweli ila nitaolewa na mzee mwenzangu ili wajukuu wapate babu,” alisema Mama Mobeto ambaye tafsiri ya maneno yake ni kama amemtupia dongo mama Esma
aliefunga ndoa hivi karibuni na kijana anayedaiwa kuwa ni Serengeti Boy kwake.

 

1481 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!