“Ikiwa unataka kupata amani na adui yako, unapaswa kufanya kazi na adui yako, kisha anageuka na kuwa mdau wako.”

Haya ni maneno ya Rais wa Kwanza wa Afrika Kusini, Nelson Mandela aliyemaliza vita ya ubaguzi wa rangi kwa kutumia mfumo wa kufanya kazi na Wazungu waliokuwa wakiwabagua Waafrika.

***

Zenawi: Vita inasaidia

“Tutazungumza wakati tukipigana. Tutapigana wakati tukizungumza. Njia yoyote inayotufikisha kwenye amani haraka ndiyo njia tutakayoifuata”.

Haya ni maneno ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Ethiopia, Meles Zenawi, aliyefariki wiki iliyopita.

**

Mills: Umoja kwanza

“Kama binadamu, tunapata mafanikio makubwa tunapoishi kwa mawazo ya kuwa wamoja badala ya kugawanyika na tunapoamua kuwa lengo moja.”

Haya ni maneno ya Rais wa Ghana John Evans Atta Mills, aliyefariki dunia hivi karibuni, katika hotuba yake aliyoitoa kwa watu wa Ghana muda mfupi baada ya kushinda urais miaka mitatu iliyopita.

***

Kennedy: Tusipende dezo

“Usiombe kupata maisha rahisi, bali omba nguvu kama mwanadamu.”

Haya ni maneno ya Rais wa Marekani John Fitzgerald Kennedy aliyeuawa kwa kupigwa risasi, alipokuwa akiwaonya watu wa taifa lake kuwa wasipende vya ubwete bali wafanye kazi.

979 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!