Balozi Feely alikifanyia kazi Marekani ya Latini kwa kipindi cha muda mrefu
Balozi Feely alikifanyia kazi Marekani ya Latini kwa kipindi cha muda mrefu

Balozi wa Marekani nchini Panama amejiuzulu kwa sababu anasema kuwa hawezi tena kuhudumu chini ya utawala wa rais Trump.

John Feely ,rubani wa ndege wa jeshi la wanamaji alisema kuwa ilikuwa na heshima kubwa kwake kujiuzulu.

Idara ya maswala ya kigeni ambayo inasimamia mabalozi wa Marekani iligundua kwamba amejiuzulu baadaye mwezi Disemba.

Kujiuzulu kwake hakukusababishwa na matamshi ya Trump ya hivi majuzi akiyataja mataifa ya Afrika na lile la Haiti kuwa ”shimo la kinyesi”.

”Kama afisa mdogo anayehusika na maswala ya kigeni, nilikula kiapo kumuhudumia rais na utawala wake hata iwapo sitakubaliana na sera kadhaa”, bwana Feely alisema katika barua yake ya kujiuzulu.

”Washauri wangu walianimbia kwamba iwapo naona siwezi kuhudumu tena basi ilikuwa heshima kujiuzulu.Wakati huo umefika”.

Katibu wa kudumu wa wizara ya maswala ya kigeni Steve Goldstein alithibitisha kwamba anajua kwamba bwana feely alitaka kuondoka kabla ya matamshi ya rais Trump ya siku ya Alhamisi.

Alisema kwamba balozi huyo ambaye alikuwa akifanyia kazi Marekani ya Latini alikuwa akiondoka kutokana na sababu zake za kibinafsi.

Baadhi ya sera za rais Trump zimesababisha hisia kali , ikiwemo hatua yake ya hivi karibuni kufutilia mbali vibali vya kuishi kwa raia wengi wa El Salvado, Haiti na Nicaragua wanaoishi nchini Marekani baada ya majanga.

Bwana Feely sio afisa wa kwanza wa wizara ya maswala ya kigeni kujiuzulu.

Elizabeth Shackeford aliehudumu mjini Nairobi kwa ujumbe wa Marekani nchini Somalia alijiuzulu mwezi Disemba.

 

By Jamhuri