Serikali ya Ethiopia inasema imemuachilia mwanasiasa maarufu wa upinzani baada ya zaidi ya mwaka mmoja kizuizini.

Kuachiliwa kwa Merera Gudina mkuu wa chama cha Oromo Federalist Congress, kunafanywa kama sehemu ya jitihada ya kutafuta uwiano wa kitaifa.

Siku ya Jumatatu mamlaka zilisema kuwa watafuta makosa kwa wafungwa 500.

Pia mamlaka zimehaidi msamaha kuwasamehe wanasiasa kadha wa upinzani walio gerezani na kufunga kizuzi maarufu cha Maekalawi.

Ethiopia imekumbwa na zaidi ya miaka miwili ya maandamano ya kuipinga serikali, mara nyingi yanayoongozwa na jamii ya Oromo, huku waandamanaji wakitaka kufanywa mabadiliko na kumalizwa kwa ukiukaji wa haki za binadamu.

By Jamhuri