Baada ya Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa kumtembelea Rais Magufuli Ikulu Jiji Dar es Salaam, na kumwagia sifa kwa jinsi anavyoiendesha nchi hasa kwenye upande wa utengenezaji wa ajira kwa vijana kwa kujenga Mioundombinu ya usafiri kama vile Reli ya Standard Gauge, utoaji wa Elimu kwa watoto wetu.

Mwenyekiti wa CHADEMA na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe amemshangaa Lowasa kwa kuisifia serikali ya Magufuli kwamba anaongoza nchi vizuri wakati kumekuwepo na matukio ya watu kuuawa na kupotea, demokrasia na haki za binadamu zinaminywa, uchumi unazidi kudidimia.

Mbowe anaendelea kumshangaa Lowassa kwa mazingira haya tunayo, tunashindwa kuelewa mtu anapata wapi ujasiri wa kuisifu serikali ya Rais Magufuli.

“Kauli iliyotolewa na Mhe. Lowassa katika ziara yake ya Ikulu, sio msimamo wa chama (CHADEMA). Chama kitafanya maamuzi kupitia vikao, na watatoa maazimio ya pamoja baada ya kutafakari na kujadiliana kwa upana wake. Mh. Mbowe alisema.

4337 Total Views 2 Views Today
||||| 1 I Like It! |||||
Sambaza!