RC Rukwa, Joachim Wangabo amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga kumchukulia hatua Mkuu wa Shule ya Sekondari Muhama kwa kuwatoza wanafunzi michango ya TZS 5,000 kama gharama ya kuwapatiwa fomu za maelezo ya kujiunga na shule hiyo.

Hatua hiyo amechukua baada ya kupokea taarifa ya kuwepo kwa michango shuleni hapo ikiwa Rais Magufuli alishapiga marufuku kuchangisha michango yoyote ile kwenye shule za serikali mpaka pale tu Wazazi wakubaliane na Walimu kuchangisha michango.

Kwa kitendo hicho cha kuchangisha michango ya fomu za kujiunga na shule, Mwalimu mkuu huyo atakuwa ameipinga kauli ya Rais Magufuli wanafunzi kutochangishwa michango shuleni.

 

1852 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!