Mjumbe wa Nyumba kumi kinondoni amgaia shillingi elfu 10, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda.

Tukio hilo limetokea leo Kinondoni ambapo Rais Magufuli alitembelea kukagua ujenzi wa Msikiti unaojengwa kwa msaada wa Kiongozi wa Morocco.
Mjumbe huyo wa nyumba kumi alipata nafasi ya kumueleza Rais kero inayomsumbua katika mtaa wake, kwamba kuna mfereji ambao unasumbua sana kipindi cha mvua hivyo alimuomba msaada rais aweze kumsaidia kutatua kero hiyo.

Papo hapo Rais Magufuli ametoa agizo mfereji huo ujengwe na ukimalizika upewe jina la mjumbe huyo ambaye anaitwa Rashidi. “Rashidi Road”
Baada ya kutoa agizo hilo Rais Magufuli alimuuliza mjumbe nyumba kumi anafanya kazi gani,
Mjumbe alijibu anauza genge ndipo Rais akampatia laki 2 papo hapo ili aongezee biashara yake,
Alivyopewa fedha hiyo mjumbe alisikika akisema mkuu wa mkoa amemuomba elfu 10 na yeye bila iana akampatia, na Mkuu wa mkoa akaitia mfukoni.

 

1222 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!