Andiko hili ni la Mwanassheria Mkuu wa Serikali (AG), Dk. Adelardus Kilangi. Aliliandika mwaka jana akiwa Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine, Tawi la Arusha.

Dk. Kilangi kitaaluma ni mwanasheria ambaye miongoni mwa maeneo aliyobobea ni kwenye sheria za madini. Aliandika makala hii ukiwa ni mtazamo wake binafsi akichangia kwenye mjadala wa makinikia baada ya kuwasilishwa kwa ripoti ya kamati ya kwanza iliyoundwa na Rais John Magufuli.

Kwa umuhimu wake Gazeti la JAMHURI linaleta andiko hilo neno kwa neno kama alivyoandika Dk. Kilangi mwenyewe:

 

Wandugu,

  1. Nitaomba tuvumiliane. Niliombwa kusema kitu. Nitaandika kwa kirefu kidogo. Kwa kuwa ninaandika muda huu, nina advantage ya kuwa nimesoma maoni mengine yaliyotangulia. Nilicheka sana kaka yangu Ngwilimi [Godwin Ngwilimi ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika] aliposema halali hadi nimetoa maoni. Sipendi kumkosesha usingizi. Nitaandika kwa paragraphs ili kurahisisha rejea.
  2. Nimeangalia maoni mbalimbali yaliyotolewa humu. Yanagusa maeneo yafuatayo:
  3. i) Statement ya Acacia.
  4. ii) Suala la sovereignty over natural resources na tatizo la ‘state capture’.
  5. ii) Suala la smelting na mchanga wa makinikia.
  6. iv) Nini tunaweza kufanya kwenye mikataba:

– kuvunja mikataba?

– kushitaki kwa kutuibia?

– ku-review mikataba?

– au kuweka mikataba wazi?

  1. vi) Sheria za kimataifa.
  2. Haya ni mambo mengi na mazito. Sio rahisi kuya-summarize kwenye text ya simu. Pia ni vema kukubaliana kuwa kwenye mjadala kama huu itikadi, vyama na mihemko iwekwe pembeni. Hoja zitawale.
  3. Sitaingia kwenye mtego wa kulaumu au kutetea mtu. Nitajikita kwenye masuala ya msingi yanayotengeneza chimbuko la tatizo. Matatizo katika sekta yetu ya madini, kama ilivyo katika nchi nyingi zinazoendelea, nyingi zikiwa Afrika, na Tanzania ikiwemo, yana chanzo chake katika maeneo matatu:
  4. i) Falsafa inayotuongoza.
  5. ii) Sheria inayotuongoza.

iii) Mfumo wa utawala.

FALSAFA INAYOTUONGOZA

  1. Malalamiko kuwa nchi zinazoendelea na zenye kumiliki resources zinapunjwa hayakuanza leo. Yalianza miaka ya 1950. Haya yalipelea kuibuka kwa falsafa mbili: resource nationalism na resource liberalism. Kila moja ina implications kwenye sheria na kwenye namna nchi itasimamia raslimali zake.
  2. Wale wa resource nationalism walitaka nchi iwe na mamlaka kamili kwa resources zao na ziwasaidie na wakatengeneza principle ya permanent sovereignty over natural resources. Walitaka mambo haya yasimamiwe zaidi na sheria za nchi.
  3. Wale wa resource liberalism wanataka raslimali ziwe wazi kwa dunia nzima maana mgawanyo wake duniani hauna usawa (japokuwa wao wamelinda teknolojia yao).
  4. Katika vision ya nchi, nchi inachagua falsafa ya kufuata. Falsafa inayofuatwa huathiri sera na sheria.
  5. Baada ya Uhuru Tanzania ilifuata falsafa ya resource nationalism hadi 1979. Kuanzia 1979 Tanzania ikaanza kufuata resource liberalism baada ya shinikizo la World Bank na IMF chini ya kitu kinaitwa Washington Consensus. Falsafa hii ilifikia kilele miaka ya 1990 mwishoni. Kwa hiyo ikaathiri sera na sheria.
  6. Kuanzia mwishoni mwa miaka ya 2000 nchi imejaribu kurudi kwenye resource nationalism, lakini inakwama. Sasa hivi resource nationalism sentiments ziko very high.

SHERIA INAYOTUONGOZA

 

  1. Kama nilivyosema, falsafa huja kuathiri Sera na Sheria. Sheria muhimu hapa ni (nitachanganya lugha kidogo hapa):
  2. i) investment law
  3. ii) mining/petroleum law

iii) tax law.

Investment Law

  1. Hiki ni chanzo kikubwa cha ugomvi. Nchi zilizoendelea zimeshinikiza uwepo wa mfumo wa sheria wenye kugandamiza nchi zinazoendelea. Mfumo huu unagawanyika kama ifuatavyo na kila kipande kina matatizo makubwa na mengi.
  2. i) Customary international law: Humu kuna principles nyingi ambazo nchi inaweza kuambiwa kuwa imezivunja. Nchi zilizoendelea na zinazoendelea zinagombana juu ya principles
  3. ii) Multilateral framework: Hapa kuna mikataba ya mataifa mengi. Tanzania ni mwanachama wa mikataba miwili yaani unaoanzisha Multilateral Investment Guarantee Agency (MIGA) na unaoanzisha International Centre for the Settlement of Investment Disputes (ICSID).

iii) Bilateral framework: Hii ni mikataba kati ya nchi na nchi (bilateral investment treaties – BITs. Ila inawalinda wawekezaji toka nchi hizo mbili. Nchi inaweza kushindwa kesi sio sababu ya mikataba ila kwa sababu ya BITs.

 

  1. iv) National framework (mining and petroleum acts): Hizi zina certain aspect fulani za investment.
  2. v) State-investor agreements (tunayoita mikataba na wawekezaji).

Wengi tunaangalia hii tu. Hatuangalii hizo frameworks zingine ambazo baadaye zinatukandamiza.

Pia, framework No. i, ii, na iii ziko chini ya himaya ya sheria za kimataifa.

 

Mining/petroleum law

  1. Mining and petroleum law hutengenezwa na nchi yenye resources. Lakini nchi zilizoendelea huwa zina-influence mno zoezi la utengenezaji sheria hizi, maana hizo ndio hutoa mineral or petroleum rights. Wako tayari hata kuidanganya nchi kwa misaada wanayojua tunahitaji sana. Wanaweza kutudanganya kuwa wanatupatia technical support. Kumbe wanatutengenezea sheria itakayowezesha kutuibia.

Tax Law

  1. Tax law ni eneo jingine ambalo linatumika sana kutuibia. Mnapokuwa mnatengeneza sheria zenu za kodi hawa jamaa hawaachi kuwazungukieni na kuwa-influence.

MFUMO WA UTAWALA

  1. Kuna tatizo kubwa sana linalozikumba hasa nchi za Africa na baadhi ya zinazoendelea zilizo nje ya Afrika. Hili ni tatizo la ‘state capture’. Kama ilivyo concept ya ‘river capture’ kwenye geography, basi state capture means influence by the elite or business people or investors such that the state (led by its government) fails to think on its own and it follows the thinking of the group that has captured it.
  2. Wakati wa kufuata falsafa ya resource liberalism, Tanzania iliingia kwenye total ‘state capture’. Ndio kusema tuliondoa kichwa chetu tukaweka kichwa kingine. Tukawa tunafikiri kwa mfumo wa hicho kichwa kingine. Sasa tumeanza kurudisha kichwa chetu.

SUALA LA MCHANGA WA MADINI

Utangulizi

  1. Suala hili wote tunajua background yake. Kamati ya pili natumaini itafanya kazi yake na uchambuzi wa kutosha.

Mchanga kwenye madini ni mali ya nani?

  1. Principle ya ‘permanent sovereignty over natural resources inasema huu ni mali ya nchi. Article 27 of the Constitution of the URT inachukua mwelekeo huo huo. Hata Section 5 of the Mining Act says the same. And the same position was in Mining Acts za 1998 na 1979. Zile za kabla ya hapo zilikuwa zinazungumzia Mwingereza.
  2. Hata hivyo kuna ubishi kuwa pale nchi inaposaini state-investor agreement (Mineral Development Agreement) na kutoa mineral rights je, nchi inakabidhi sovereignty yote kwa companies. Makampuni yatasema ‘ndiyo’. Nchi zinatakiwa ziseme ‘hapana’.
  3. Mineral rights means rights to extract minerals and sell them. Does it include transporting them outside the country in order to extract minerals? I don’t think if contracts say so. And if they do, that defeats the principle of permanent sovereignty over natural resources!

 

Nini Tunaweza kufanya kuhusu mikataba?

  1. Kuivunja? Hatuwezi kuivunja. Tumesaini mkataba wa MIGA na wa ICSID. Tutashtakiwa kwa kuvunja customary law principle ya ‘fair and equitable treatment’, na ‘state responsibility’ na ya ‘respect for acquired rights’. Tutapelekwa mbele ya ICSID na kuhukumiwa, kisha tutaminywa na MIGA itakayokamata mali zetu popote zilipo.
  2. Kushitaki makampuni kwa kutudanganya? Tunaweza, na tutatumia argument kuwa wamevunja customary law principle ya ‘good faith and prohibition of abuse of rights’. Lakini wakisema uchunguzi wa mchanga tumeufanya kwa upande mmoja wanaweza kushinda.
  3. Ku-review mikataba? Lazima tuwe tume -incorporate kwenye mkataba kipengele kinachohusiana na doctrine ya ‘clausula rebus sic stantibus’. Hii ni doctrine inayoruhusu ku-review mkataba kama conditions fulani zikibadilika. Lazima kifungu hiki kiwe kwenye mikataba. Hawa jamaa walihakikisha hakimo kwenye mikataba yetu. Kwa hiyo ukianza process ya ku-review unilaterally watasema umevunja principle ya ‘fair and equitable treatment’.
  4. Kuiweka wazi mikataba ili watu wote waione? Investors wataegemea kwenye principle of confidentiality of investment agreements. Hii principle IPO katika international law. Ingawa sasa kuna mabishano makubwa. Wengine wanaipinga. Ndio maana japokuwa tuna sheria mpya ya uwazi na uwajibikaji – Extractive Industries (Transparency and Accountability) Act, 2015, ambayo inasema mikataba yote iwekwe wazi, makampuni yamekataa kwa kusema kuwa wakati wanasaini mikataba hiyo sheria hiyo haikuwepo. Mnavyojua sheria hairudi kinyume. Kumbe watadai bado canal in sea na principle hiyo.
  5. Kwa hiyo kumbe tunaweza kufanya nini sasa? KAMA ALIVYOSEMA MHESHIMIWA RAIS, HII VITA, NA HII NILIYOTOA HAPA NDIO PICHA HALISI YA VITA HII.

Basi wandugu siku nyingine msinitafute ili nitoe maoni yangu. Vinginevyo mjiandae kusoma kitabu.

By Jamhuri