MAREKANI : Mtoto wa umri wa miaka miwili nchini Marekani amefariki baada ya kujipiga risasi kichwani kwa bunduki ambayo imekuwa ikihifadhiwa na wazazi wake nyumbani kwao.

Polisi wa Houston, Texas wanasema wazazi wa mtoto huyo – Christopher Williams Jr – walikuwa nyumbani wakati wa kutokea kwa kisa hicho.

Polisi wanasema bunduki hiyo ambayo hutumia risasi za ukubwa wa 9mm ilipatikana eneo la tukio na kwamba ilikuwa inamilikiwa na babake.

Kufikia sasa, bado haijabainika iwapo wazazi wake watashtakiwa.

By Jamhuri