Nawapongeza kwa ujasiri mlioamua kuuvaa katika harakati bila shaka ni lengo lenu ni kuona Mtanzania ananufaika na maliasiri tulizojliwa na Mungu.
Hawa jamaa matapeli na wauza ‘unga’ mlioamua kufichua maovu yao tunajua kuwa wana nguvu nyingi za kibinadamu, lakini tuna imani ninyi mpo na Mungu, cha muhimu tunawaomba mchukue tahadhari kubwa popote mnapokanyaga miguu yenu.
Asanteni sana na kwa niaba ya Watanzania wasiyo na uwezo au muda wa kuwasiliana nanyi kwa njia yeyote ile basi tunawatakia kazi njema watu wa Jamhuri na Mungu awe nanyi daima.
Email: justineshija@yahoo.com

 

1319 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!