Julius Nyerere: Nchi haiendelei bila viwanda vya kisasa

“Maana ya maendeleo ya leo ya uchumi wenye nguvu ni maendeleo ya viwanda. Nchi yenye viwanda tunasema ni nchi iliyoendelea. Hata hivyo, tuna maana nyingine ya nchi zilizoendelea ya kuziita ni nchi zenye viwanda. Nchi haiwezi kuendelea bila kuwa na viwanda vya kisasa.

Maneno haya ni ya Baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Ndiye Rais wa kwanza wa Tanganyika na baadaye Tanzania.

Kamala Harris: Nimelelewa kuwa mwanamke wa kujitegemea

“Mama yangu alikuwa na msemo: ‘Kamala, wewe huenda utakuwa wa kwanza kufanya vitu vingi, lakini hakikisha hauwi wa mwisho.’ Nimelelewa kuwa mwanamke anayejitegemea, siyo mhanga wa kitu chochote.

 

Haya ni maneno ya mwanasheria maarufu wa nchini Marekani, Kamala Davi Harris, ambaye kwa sasa ni Mwanasheria Mkuu wa 32 wa Califonia, Marekani.

 

Manmohan Singh: Ubepari ni nguvu ya maendeleo mapya

“Ubepari kihistoria umekuwa wa nguvu nguvu sana, na nyuma ya nguvu hiyo ni maendeleo ya kiufundi, uvumbuzi, mawazo mapya, bidhaa mpya, teknolojia mpya, na mbinu mpya za kusimamia timu.”

 

Kauli hii ni ya Waziri Mkuu wa 13 wa India, Manmohan Singh. Ndiye Kalasinga (kabila la Wahindi wanaofuga ndevu na nywele na kuvaa kilemba; singasinga) wa kwanza kupata wadhifa huo nchini India.

 

Margaret Chan: Tumbaku ina faida kubwa lakini inaua

“Tumbaku ni sekta pekee ambayo huzalisha bidhaa kutengeneza faida kubwa na wakati huo huo kuathiri afya na kuua watumiaji.”

 

Hii ni kauli ya Margaret Chan Fung Fu-chun, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO). Alizaliwa mwaka 1947 huko Hong Kong, China.

 

By Jamhuri