Julius Nyerere: Serikali imiliki mashirika nyeti

“Mashirika ya msingi na nyeti kwa maendeleo ya taifa kama bandari, reli, posta na simu, nishati na mabenki ya umma yaliyopo, yaendelee kumilikiwa na dola. Wananchi wataweza kuuziwa sehemu ya hisa katika mashirika hayo na mashirika haya yanaweza kuingia ubia na makampuni binafsi, mradi tu kwa uwiano unaolifanya shirika kuendelea kuwa la dola.”

Maneno haya ni ya Baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

 

Yingluck Shinawatra: Nitatenda haki kwa kila mtu

“Nitafanya kila kitu kwa kuomba uhalali na kwa kuomba utawala wa sheria. Na kitu kikubwa muhimu ninapaswa kumtendea haki kila mmoja, siyo tu kwa mtu mmoja pekee.”

 

Kauli hii ni ya Waziri Mkuu wa 28 na wa sasa wa Thailand, Yingluck Shinawatra.

 

Vladimir Putin: Anayeshabikia Sovyeti hana akili

“Mtu yeyote ambaye hajutii Muungano wa Kisovyeti uliopita hana moyo. Mtu yeyote anayetaka muungano huo urejeshwe hana akili.”

Maneno haya ni ya Rais wa Urusi, Vladimir Vladimirovich Putin. Alipata kuwa Waziri Mkuu wan chi hiyo kati ya mwaka 1999 na 2000.

 

Sri Indrawati: Mwanamke anaongoza maendeleo ya kiuchumi

“Utafiti wa kina uliofanyika unaonesha kwamba mwanamke ana mazingira magumu zaidi lakini pia ana nguvu kubwa ya kuongoza maendeleo ya kiuchumi.”

Haya ni maneno ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia (WB) nchini Indonesia, Sri Mulyani Indrawati.

 

 

1631 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!