JAMHURI limetufumbua macho

Nawapongeza na kuwapa pole wana JAMHURI. Ni kweli vitisho vipo na vitazidi kuja, ila Watanzania wengi tuko nyuma yenu. Mtambue kuwa kugusa mfumo (corrupt syndicate) si lelemama. Watanzania wengi gazeti hili limetufumbua macho. Niwaombe Watanzania wenye nia njema tuzidi kumwomba Mungu ili ukweli uendelee kushinda.

Albert Mwombe (ADVOCATE), Lindi

0688 405 748

Kero ya maji Morogoro

Tatizo la uhaba wa maji litaisha lini Morogoro vijijini? Utekelezaji mbovu wa mabomba ya maji unadhihirika wazi. Mbunge na diwani wameshindwa kushughulikia kero hiyo. Vijiji vinavyokumbwa na tatizo hilo ni Kidugalo, Sanga, Ngerengere, Ubena na Kizuka. Tunaomba Rais aingilie kati suala hili.

Msomaji wa JAMHURI, Morogoro

0652 435 768

 

Kagame amezoea matusi

Wasiomjua Kagame [Rais wa Rwanda, Paul Kagame] wafahamu kuwa siyo mara yake ya kwanza kuwatukana wakuu wa nchi nyingine, hasa wanapomshauri juu ya jambo fulani. Amepata pia kumtukana Rais wa Afrika Kusini, Tabo Mbeki na Rais wa Ufaransa. Ninampongeza Rais wetu [Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete] kwa kukwepa malumbano na Kagame.

 

Benedict Sikwara

0687 057 387

 

Msongamano wa abiria

Nashauri Serikali idhibiti msongamano wa abiria kwenye magari, hasa kwenye daladala za jijini Dar es Salaam kwani hali hiyo inachangia kueneza ugonjwa hatari wa kifua kikuu. Lakini pia hali hiyo inahatarisha usalama wa abiria na magari husika wakati wa ajali. Serikali ilitupe macho suala hili.

 

Ismaili Juma, Lushoto – Tanga

0656 744 166

 

Tusikurupuke wahamiaji haramu

Kumuita mtu mhamiaji haramu kwa sababu tu ana pua ndefu au kwa sababu anaongea Kinyarwanda ni uonevu. Hivi kila anayeongea Kiingereza apelekwe Uingereza? Anayeongea Kihausa apelekwe Ghana? Anayeongea Kichina apelekwe China? Vitambulisho rasmi vya Taifa vitatuepushia tatizo hilo.

 

Mjalabu Gervas Bugambage Rutaguzinda

0657 576 646

 

Naibu Spika ajirekebishe

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, licha ya ukereketwa wake kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ana haiba yake binafsi isiyofaa kwa uongozi. Tabia yake ni ya hamaki na ubabe inayotokana na kutojiamini, na yeye ndiye amekuwa akisababisha vurugu nyingi bungeni.

 

Berto Mdendemi

0767 046 123

 

Airtel kuweni waungwana

Baadhi ya wamiliki wa kampuni za mitandao ya simu za mkononi sasa hivi ni wezi wa kupindukia. Kwa mfano, Septemba 11, 2013 nilijiunga na Airteli Yatosha na kupata dakika 20 za kuongea. Cha ajabu nilimpigia mtu nikaongea naye kwa muda wa dakika moja na sekunde 34 simu ikakata eti salio limekwisha! Kama siyo wezi nisemeje?

Naitwa Gemos

0784 864 555, 0754 832 094

 

 

Pongezi Dk. Mwakyembe

Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, ataweza kuzuia unga [dawa za kulevya]? Tanzania kwa miaka mingi sasa inaonekana kuwa jalala la dawa za kulevya. Hii ni kutokana na baadhi ya viongozi katika nchi hii kulifumbia macho suala hili na huenda wananufaika nalo. Hata hivyo, sisiti kumpongeza Dk. Mwakyembe kwa utendaji kazi wake mzuri.

 

Mathias Rwegasira, Dar es Salaam

0787 918 384

 

By Jamhuri