Julius Nyerere: Nina haki ya kupiga na kupigiwa kura

 

“Watanzania wengine hawamo CCM, hawapo wapi na hawana chama chochote. Hata hivyo, nikikataa kuingia katika chama isiwe sababu ya kuninyang’anya haki yangu ya kupiga na kupigiwa kura. Ninayo tu na naweza nikaamua kuitumia mwenyewe tu.”

 

 

Maneno haya ni ya Baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais wa kwanza wa Tanganyika na baadaye Tanzania.

 

Amy Adams: Tusiwapuuze wenye mtazamo chanya

“Nafikiri muda mwingi hatuwi makini kwa watu wenye mtazamo chanya kwa sababu tunadhani hawajui au ni wajinga au hawakusoma.”

 

Hii ni kauli ya mwigizaji na mwimbaji maarufu wa nchini Marekani, Amy Lou Adams, ambaye pia ni miongoni mwa wanawake warembo zaidi duniani.

 

Martin Luther: Akili jumlisha tabia diyo elimu ya kweli

“Kazi ya elimu ni kufundisha mtu kufikiri kwa kina na kufikiri kwa umakini. Akili jumlisha tabia- hilo ndilo lengo la elimu ya kweli.”

 

Kauli hii ni ya padre na mwanaharakati wa nchini Marekani, Martin Luther King, Jr. Anajulikana zaidi kutokana na jukumu lake katika maendeleo ya haki za kiraia.

 

Atifete Jahjaga: Serikali ihudumie wananchi kwa haki

 

“Lazima tukumbuke kwamba demokrasia hufanya kazi wakati inapopewa muda wa kuendelea, kukomaa na kuzaa. Taasisi za serikali lazima zihudumie wananchi kwa haki, na kwa heshima, wakati wa kujibu mahitaji yao.”

 

Haya ni maneno ya Rais wa nne wa Jamhuri ya Kosovo, Atifete Jahjaga. Ni mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo nchini humo.

 

2198 Total Views 2 Views Today
||||| 1 I Like It! |||||
Sambaza!