Haya ni maneno aliyoyasema Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika siku ya maadhimisho ya miaka 40 ya Uhuru Ghana, jijini Accra, mwaka 1997. Alizitaka nchi za Afrika kuungana kuwa na nguvu ya kiuchumi na sauti kubwa zaidi kwani pamoja na kuwa na mataifa 53, bado ni bara linalopuuzwa duniani.

Magufuli: Wakandarasi wamekula sumu

“Wakandarasi walioamua kula fedha za miradi ya maji wajue kuwa wamekula sumu.”

Haya ni maneno ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli aliyesema fedha ya Serikali huwa hailiwi, hivyo wakanadarasi wanaojua kuwa wemekuala fedha za maji waende wenyewe kujenga miradi kama siyo warudishe fedha walizochukua na wasipofanya hivyo wakamatwe. Kauli hii ameitoa wiki iliyopita.

Mugabe: Tuitumie taulo vizuri

“Unapojifuta maji bafuni, itumie vizuri taulo, maana sehemu unayoitumia kufuta makalio inaweza kupita mdomoni pako.”

Hii ni moja ya kauli maarufu aliyoitoa Rais (mstaafu) wa Zimbabwe, Robert Gabriel Mugabe alipokuwa akiwaasa watu wake kutotukana mamba kabla hawajavuka mto mwaka 1980 wakati nchi yake inapigania uhuru.

Yoweri Museveni: Kukaa serikalini

“Baadhi ya watu wanadhani kukaa serikalini muda mrefu ni jambo baya, lakini kadri unavyokaa zaidi, ndivyo unavyojifunza zaidi. Kwa sasa mimi ni bingwa wa uongozi.”

Hii ni kauli ya Rais wa Uganda, Yoweri Museveni aliyoitoa mwaka 2017 wakati nchi yake ilipokuwa na vuguvugu la kubadili Katiba ya Uganda kuondoa Ibara iliyokuwa inaweka ukomo wa umri kwa mtu kugombea urais.

1403 Total Views 1 Views Today
||||| 1 I Like It! |||||
Sambaza!