AJALI : Watu 3 wamefariki dunia na wengine 5 wamejeruhiwa katika ajali ambayo imetokea jioni hii eneo la Boko Magengeni Manispaa ya Kinondoni ajali hiyo imehusisha magari matatu ikiwemo gari la kubebea michanga na basi la wanafunzi

Mkuu wa Trafiki Wilaya ya Kawe Inspekta msaidizi wa Polisi Makame akizungumza na TV E,/ Efm habari amethibitisha na kusema miili ya Marehemu imepelekwa kuhifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya Mwananyamala ambako pia majeruhi wamepelekwa kwa ajili ya matibabu, wengine wamepelekwa hospitali ya Lugalo.

By Jamhuri