Kumefanyika mazishi ya wapiganaji wa Kikurdi waliouawa katika operesheni ya vikosi vya Uturuki mjini Afrin

Maelfu ya watu katika mji uliodhibitiwa na wakurdi Afrin, kakazini mwa Syria wamefanya maandamano kupinga mashambulizi yanaoendeshwa na Uturuki.

Uongozi wa ndani wa eneo hilo, wametoa tamko kwa mataifa ya nje kusaidia kusimamisha mapigano hayo, na wameishutumu Urusi kuhusika na yanayoendelea eneo hilo.

Ngoma zikipigwa, huku wakibeba mabango yenye ujumbe, waandamani hao wanaonesha hasira walizonazo juu ya kitendo cha uturuki cha kuanzisha operesheni ya kijeshi katika eneo hilo la kaskazini

maelfu ya watu wamehama makazi yao kutokana na operesheni hiyo ya uturuki, afisa wa afya wa kikurdi alisema kuwa watu 150 waliuawa na wengine 300 kujeruhiwa tangu kuanza kwa operesheni ya uturuki,

Operesheni ya uturuki huko mkoa wa Afrin imetokana na uturuki kuwashutumu kundi la Kikurdi kuwa ni kundi la kigaidi, na wanashirikiana na chama cha wafanyakazi cha kikurdi kilichopigwa marufuku Uturuki.

Uturuki imesema kuwa imewatuma wanajeshi zaidi hadi Afrin ili kuwafurusha wanamgambo wa Kikurdi

Mataifa yenye nguvu kama Marekani na Ufaransa walitoa wito kwa Uturuki kusitisha mapigano hayo.

Kutokana na operesheni hiyo, Uturuki nayo ilipata pigo la kuuwawa kwa wanajeshi wake saba kutokana na shambulio lilofanywa na kundi la Kikurdi dhidi yao.

Katika taarifa kutoka idara ya jeshi la Uturuki, wapiganaji wa kundi la Kikurdi la YPG walishambulia kwa makombora kifaru moja ya jeshi lake katika eneo la Sheikh Haruz, Kaskazini Mashariki mwa mji wa Afrin.

Waziri mkuu wa Uturuki Binali Yildirim alisema kuwa kikundi hicho cha Kikurdi watalipa kutokana na shambulio walilolifanya.

Operesheni ya Uturuki ilianza mapema mwaka huu, dhumuni kuu ikiwa ni kuwaondoa kabisa wapiganaji wa Kikurdi.

1062 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!