MAONI YA WASOMAJI KATIKA BLOG

……….
Heee, hii kamati (Tume) Mr. President iko very biased. Mwenyekiti na Naibu wake ni ‘me’, angalau Katibu wa Sekretarieti angekuwa ‘ke’. Lakini umechagua yote madume, akina mama wakale wapi na siku hizi wamesoma?

***

Tunampongeza sana Mheshimiwa Rais kuteua Tume hii kwa wakati mwafaka chini ya uenyekiti wa Jaji Warioba, Makamu Jaji Mkuu mstaafu Ramadhani, wanazuoni nguli wa Katiba – Dk. Sengondo, Profesa Kabudi, Profesa Baregu, wanasiasa wakongwe Dk. Salim, Butiku, Fatma Said Ali; na wanajamii waliomo tunawaaminia!

***

Profesa Lipumba naona angeongezwa kutoa mchango wake hapo vile vile.

***
Imetulia

***

Baregu ndani ya nyumba, nimeikubali hii

***

Timu imekamilika, hongera Mheshimiwa Rais na pole kwa kazi hii nzito. Mwenyekiti wa Tume swadakta. Lakini naona tu wanawake Bara “underrepresented”- sema hao waliopita tuna imani watatuwakilisha vyema. Na kwa nini Zanzibar na Bara iwe na idadi ya wajumbe sawa wakati wananchi wa Zanzibar idadi ni ndogo na Bara ina idadi kubwa ya watu?

***

Kimsingi azma imetimia japokuwa dhana ya uundaji wa Tume huru haijatimia.
[1]. Tulitarajia kama alivyoahidi Mheshimiwa Rais ushiriki wa makundi mbalimbali ya kijamii ungedhihirika ndani ya hii Tume, lakini hilo nadhani halikuwezekana.
Hatujaona kiongozi wa madhehebu ya kiroho ndani ya Tume, hatujaona ushiriki wa wanasiasa wenye busara zao nje ya chama tawala, hatujaona ushiriki wa wanawake ulio sambamba na mabadiliko ya kisiasa, kiuchumi, na kiutamaduni, hatujaona ushiriki wa Watanzania kutoka chombo cha kutunga sheria, hatujaona ushiriki wa Watanzania sekta ya biashara na kadhalika.
Kwa busara zangu, “in a long run” itaibuka mitazamo ya “biased formation of this Constitutional Re-construction Commission” kutoka kwa makundi ya kijamii ambayo hayakushirikishwa.

[2] Tulitegemea pia kwamba chanzo cha habari hii kwa kushirikiana na Sekretarieti ya Ikulu, kuainishwa kwa taaluma, uzoefu, wadhifa na utaalamu wa wajumbe wa Tume ili kukidhi dhana ya utawala bora chini ya kipengele cha “transparency” kama ambavyo ilidhaniwa kutoka mwanzo.

[3] Kwa mshangao mwingine tunashindwa kujua kama hili linafanywa makusudi, ama kwa bahati mbaya, au kutojua. Ikulu ni “Autonomous Entity” ambayo ina mifumo maalumu ya utoaji wa taarifa kwa umma. Kwa mara nyingi, Mkurugenzi wa Mawasiliano anatumia “blog” zisizo rasmi na halali bila kuzingatia itifaki ya kanuni na taratibu za Ikulu katika utoaji wa taarifa. Mathalani, taarifa hii utaiona kwenye blog kabla ya kuiona kwenye gazeti la serikali, utaanza kuiona kwenye website binafsi kabla ya kuiona kwenye blogu na website ya Serikali.
Ushauri: Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu kuweni “serious na protocol” ya hiyo “autonomous entity.”

[4) Mwisho, ni matumaini ya Watanzania kuwa pamoja na mapungufu (upungufu) yaliyoanza kujitokeza awali juu ya uundwaji wa hii Tume, ufanisi, weledi, uelewa, busara, hekima, ukweli na uwazi vitakuwa nguzo ya upatikanaji wa Katiba ya Milenia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika.

Mdau,
Joachim K. Global.

***

Mbona kamati hii viongozi wa juu wote ni CCM?

***

Sina wasiwasi na Tume, the way ninavyoichukia CCM, hapo JK ameweka u-CCM kando. Nusu ya timu ni watu wenye uchungu na nchi. Jamani nafasi ya kujikomboa ndiyo hii, Mungu atupe nini tena. Mungu ibariki Tanzania na watu wake.

***

Ingawa hawezi kuridhisha kila mmoja wetu, kamati (Tume) ipo balanced ila vijana siwaoni humo inakuwaje?

****

Kuna mtu kama Profesa Issa Shivji, bingwa wa sheria kuachwa haingii akilini. Kuna kina Profesa Safari, kina Nkono nadhani Tume imelenga siasa zaidi kuliko hatima ya Watanzania. Yetu macho, bali Tume itambue kuwa hatima ya safari yetu kwenye nchi ya matunda na maziwa ipo mikononi mwao. Mungu ibariki Tanzania na watu wake.

Mdau Loliondo.

 

2836 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!