Kikosi cha Ruvu Shootinga kimeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Uwanja wa Mabatini, Mlandizi jana.

Mchezo umepigwa jana baada ya kuahirishwa juzi Alhamis kufuatia mvua kali kunyesha iliyosababisha maji kujaa Uwanjani.

Mabao ya Ruvu yamefungwa na Khamis Mcha katika dakika ya 29 kipindi cha pili huku bao la pili likifungwa na Fully Maganga kwenye dakika ya 80 kipindi cha pili.

Katika dakika ya 74 ya mchezo, beki Aggrey Moris alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kupokea kadi ya pili ya njano na kuwafanya Azam kuwa pungufu.

Matokeo hayo yameifanya Ruvu Shooting kupanda mpaka nafasi ya 7 ya msimamo huku Azam ikishindwa kuishusha Yanga kwa kusalia katika nafasi ya 3 ikiwa na alama zake 45.

2244 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!