Wachezaji wa TP Mazembe (DRC), Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wametajwa kuwa ndiyo wachezaji watakaongoza Jahazi la timu ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, kutwaa Kombe la Chalenji mwaka huu.

Tangu kujiunga kwa wachezaji hao katika timu hiyo kumeonesha kung’ara. Samata  aliisaidia Stars kufunga goli pekee kwa kichwa katika dakika ya saba ya mchezo huo, akiunganisha krosi maridadi ya mshambuliaji mwenzake wa TP Mazembe, Ulimwengu.

Samata yuko katika orodha ya wachezaji 25 walioteuliwa na Shirikisho la Kandanda barani Afrika (CAF) kuwania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika mwaka huu kwa mchezaji bora wa Afrika anayechezea vilabu vya barani Afrika.

Timu ya Kilimanjaro imetinga nusu fainali ya michuano hiyo baada kufuta uteja kutoka kwa Timu ya Taifa ya Ukraine kwa kushinda kwa penati 3-2 baada ya kutoka sare ya 2-2.

Mwaka jana Uganda iliifunga Kilimanjaro Stars kwa mabao 3-1 katika machezo ulifanyika nchini humo.


1282 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!