SERIKALI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA TUCTA KUONGEZA TIJA NA UFANISI SEKTA YA KAZI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira,Vijana na watu wenye ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya serikali na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA) wakati alipokutana na shirikisho hilo leo tarehe 7 Januari 2018, jijini Dar es salaam. Kushoto ni Rais wa TUCTA, Tumaini Nyamghokya na kulia kwake ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais utawala bora, George Mkuchika, Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi na Ajira), Anthony Mavunde.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira,Vijana na watu wenye ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya serikali na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA) wakati alipokutana na shirikisho hilo leo tarehe 7 Januari 2018, jijini Dar es salaam.
Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA), Tumaini Nyamghokya akifanunua masuala ya wafanyakazi wakati walipokutana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira,Vijana na watu wenye ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama leo tarehe 7 Januari 2018,jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi na Ajira) Erick Shitindi akieleza masuala ya sekta ya kazi wakati wa mkutano wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA) na serikali leo tarehe 7 Januari 2018 ,jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA) na serikali wakifuatilia majadiliano ya mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, leo tarehe 7 Januari 2018 ,jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA) na serikali wakifuatilia majadiliano ya mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, leo tarehe 7 Januari 2018 ,jijini Dar es Salaam.

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira,Vijana  na watu wenye ulemavu) Mhe.  Jenista Mhagama amesema serikali itaendelea  kushirikiana na Shirikisho la Vyama vya  Wafanyakazi Nchini (TUCTA) katika kuleta tija na ufanisi katika sekta ya kazi kwa kushughulikia masualaya wafanyakazi nchini

Waziri Mhagama ameyasema hayo jana tarehe 7 Januari 2018, jijini Dar es salaam wakati wa mkutano wake na viongozi hao wa TUCTA, walipokutana kwa ajili ya kujadiliana na kushauriana juu ya mazingira bora na wezeshi ya wafanyakazi, sekta ya kazi na ajira  nchini .

“Hatuwezi kupata tija na ufanisi katika sekta ya kazi bila vyama vya wafanyakazi  kushughulikia  malalamiko na manunguniko ya wafanyakazi katika maeneo yao ya kazi hasa katika mikataba  ya ajira na stahiki zao kwa mujibu wa sheria .TUCTA msipo simamia haya hata serikali tutashindwa kutimiza wajibu wetu kikamilifu. Serikali itaendelea kushughulikia masuala  ya wafanyakazi na sekta ya kazi kwa kuzingatia miongozo, kanuni na sheria za kazi  na ajira katika kutafuta suluhu ya masuala  ya kazi” alisema Mhagama.

Mhagama aliwahakikishia TUCTA kuwa serikali itayashughulikia madai yote ya wafanyakazi ambayo yanazingatia  sheria. Aidha Mhagama aliwataka TUCTA kuvitaka vyama vya wafanyakazi kufanya vikao na wafanyakazi katika maeneo yao ya kazi  na wawapatie elimu juu ya masuala ya kazi ikiwa ni pamoja na kuwaelimisha juu ya tafsiri sahihi ya sheria za kazi  tulizonazo nchini.

Kwa upande wake Rais wa TUCTA, Tumaini  Nyamghokya ameishukuru serikali kwa ushirikiano wanaoupata toka serikalini  kupitia majadiliano ambayo yamesaidia  migogoro ya wafanyakazi kupungua katika maeneo ya kazi.  ushirikiano huo umekuwa ni mhimili mkubwa kati ya serikali, waajiri na wafanyakazi.

Mkutano huo  ulihudhuriwa  na Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi  utawala bora, George Mkuchika, Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazina Ajira), Anthony Mavunde na Katibu Mkuu Tawala za mikoa na Serikali za mitaa  na Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi na Ajira)  Erick Shitindi.

Msingi wa serkali na Shirikisho la Vyama vya  Wafanyakazi Nchini (TUCTA) kukutana kwa majadiliano na mashauriano unatokana na nchi ya Tanzania kusaini mikataba ya Shirika la Kazi Duniani (ILO), ukiwemo mkataba namba 98 wa mwaka  1949,ndio uliweka mazingira hayo  ya serikali,waajiri na wafanyakazi kukutana ili kuweka dhana ya kuaminiana na  kuleta tija na ufanisi katika sekta ya kazi na ajira.