Serikali kununua mabehewa ya kisasa 1590

Mkurugenzi Mkuu, Idara ya Habari – Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi amesema kuwa serikali imeendelea kutekeleza mafanikio na miradi mbalimbali mikubwa Kitaifa.

Akizungumza na wanahanari leo, Dkt. Abbas amesema kuwa pamoja na hayo yote miradi ikiwa ni pamoja na hali ya uchumi, Ahadi ya kuhamia Dodoma, viwanda, miradi mikubwa ya umeme, ujenzi wa reli ya kisasa()Standard Gauge, Ununuzi Mabehewa, Meli Mpya.

“Sisi kama serikali hatutaki kusubiri kwamba reli imekamilika tunaanza kuhangaika treni ziko wapi mabehewa yako wapi ya kisasa namkumbuke kuwa hii reli itakuwa yenye capability yenye uwezo wa namna mbili kwanza zitapita treni za umeme lakini kuna treni mpya za kisasa za aina ya diesel,” alisema Dkt Abbas.

“Serikali tumeanza wa kununua treni kwa maana ya treni ni mahehewa kwa maana ya vichwa vya treni ya kisasa na tukumbuke kenye ujenzi wa hii reli kutakuwa kuna jengwa na line za umeme kabisa kwasababu ni reli itakayo ruhusu mwendo wa kasi. Tumeagiza mabehewa kwenye huu ununuzi tunanuanua jumla ya mabehewa 1590 mabehewa ya kisasa na yatakuwa ya aina tofauti tofauti nataka kutolea mfano kuna haya mabehewa yaitwa Double stack containers haya yana weza kubeba container la juu na la chini na yakatembea na likafika linako paswa kufika haya ya double tumeagiza mabehewa 50.”