Home Kitaifa Hivi Ndivyo Mvua ya Ilivyosababisha Adha kwa Wananchi wa Dar es Salaam

Hivi Ndivyo Mvua ya Ilivyosababisha Adha kwa Wananchi wa Dar es Salaam

by Jamhuri

Maji yaliyokuwa yameenea sehemu ya Bonde la Mkwajuni, Kinondoni, Dar.

Maji yakitapakaa Mkwajuni.

Daraja la Jangwani lilivyoonekana kufuatia mvua kubwa ya asubuhi leo.

Foleni ndefu za magari zilizokuwa katika eneo la Jangwani kati ya Magomeni Mapipa na Jangwani.

Foleni ndefu za magari zilizokuwa katika eneo la Jangwani kati ya Magomeni Mapipa na Jangwani.

MVUA kubwa zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam na sehemu mbalimbali nchini zimeleta adha kwa wakazi wake ambapo mvua hizo zilizoanza kunyesha alfajiri leo zilisababisha foleni nyingi katika maeneo mbalimbali hasa eneo la Jangwani.

Mbali ya foleni pia mvua hizo zimesababisha mafuriko maeneo mengi ambayo mtandao huu umeyashuhudia katika bonde la Mkwajuni na Jangwani yaliyokuwa yamefurika kwa maji na tope, hali iliyosababisha watembea kwa miguu wanaotokea maeneo ya Kariakoo na mengine katikati ya jiji hilo kupita kwa tabu sehemu hizo.

You may also like