Tag Archives: gazeti la jamhuri

Yah: Nadhani tumezidi unafiki

Mara nyingi nimekuwa nikishuhudia sifa nyingi sana za mtu pale ambapo ndiyo kwanza tumemaliza kutupia chepe la mwisho la mchanga katika kaburi lake. Huwa inakuwa hotuba nzuri ya kutia simanzi juu ya uwepo wake alipokuwa hai na jinsi ambavyo nafasi yake itapata tabu sana kuzibika. Ni maneno yenye faraja ambayo kama mfu angepata nafasi ya kuyasikia, nadhani angeelewa umuhimu wa ...

Read More »

Kujitegemea – Nyerere

“Kujitegemea maana yake ni kwamba hatuna budi kutumia kwa juhudi zetu zote rasilimali yetu tuliyonayo.” Nukuu hii imetolewa kwenye kitabu cha nukuu za Kiswahili za Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere. Ubaguzi – Mandela “Ninapinga ubaguzi wa rangi kwa sababu ninauchukulia kuwa jambo la kipuuzi, iwe linatoka kwa mtu mweusi au mweupe.” Kauli hii ...

Read More »

Maandiko ya Mwalimu Nyerere: Ujamaa Sehemu ya 3

Leo Tanganyika ni nchi masikini. Hali ya maisha ya umma iko chini kiasi cha kuaibisha. Lakini kama kila mtu katika nchi, mke kwa mume, atatambua hayo na kufanya kazi ukomo wa nguvu zake, kwa faida ya nchi nzima, basi Tanganyika itaendelea; na maendeleo hayo kila mtu atayapata. Lakini mafanikio haya lazima yagawanywe kwa watu wote. Mtu mwenye kuamini Ujamaa kikwelikweli ...

Read More »

Maharamia watamba Rorya

Wizara ya Fedha imeombwa ipeleke boti wilayani Rorya, Mara ili kukabiliana na maharamia katika Ziwa Victoria. Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Simon Chacha, amesema matukio ya uvuvi haramu na biashara ya magendo vinashamiri Ziwa Victoria upande wa Rorya kutokana na kukosekana kwa boti ya doria. Amesema maharamia wakiwamo wanaotoka nchi jirani, hupora nyavu, samaki, mafuta na hata boti za wavuvi ...

Read More »

Kilichomponza tajiri Zakaria

Mfanyabiashara Peter Zakaria (58), amerejesha mali zote alizonunua kutoka Chama Kikuu cha Ushirika Nyanza (NCU), akiamini kwa kufanya hivyo ataondoa ‘nuksi’ ya kuandamwa na Serikali. Tajiri huyo mkazi wa Tarime mkoani Mara, anayemiliki vitegauchumi mbalimbali yakiwamo mabasi ya Zakaria, amekabidhi nyaraka za umiliki wa mali hizo serikalini, wiki iliyopita. Zakaria anashikiliwa rumande akituhumiwa kuwajeruhi kwa risasi maofisa usalama wawili waliomfuata ...

Read More »

Bajeti yetu, kilimo na viwanda

Balile

Na Deodatus Balile, Abuja, Nigeria Wiki hii nimekuwa hapa jijini Abuja, Nigeria. Nimepata fursa ya kukutana na Rais Mohamed Buhari wa Nigeria. Nimekutana na mawaziri wa Habari, Fedha, Viwanda na Biashara. Kukutana kwetu kumekuwa kama zari. Kilichonileta hapa Nigeria ni kuhudhuria mkutano wa mwaka wa taasisi ya International Press Institute (IPI). Kumbe Serikali ya Nigeria iliposikia kuna waandishi kutoka nchi ...

Read More »

Kasoro uhawilishaji mashamba Kusini

SONGEA NA MUNIR SHEMWETA   Uwekezaji ni jambo muhimu hasa katika kipindi hiki cha Serikali ya Awamu ya Tano ambayo msisitizo wake mkubwa ni Serikali ya Viwanda na kuelekea katika uchumi wa kati.   Hali hiyo inatokana na uwekezaji kuwa kitu kinachoweza kusaidia upatikanaji huduma muhimu sambamba na kutoa fursa ya ajira kwa wananchi na kubiresha maisha yao.   Katika ...

Read More »

Upangaji kabla ujenzi wa jengo kukamilika

NA BASHIR YAKUB Sehemu nyingi za mijini utaona majengo marefu na makubwa ambayo yamekuwa yakijengwa, mengi ya majengo hayo huwa yanapangishwa hata kabla ya ujenzi wake kukamilika. Mengine hupangwa hata kabla ya ujenzi kuanza, watu hutizama tu ramani ya jengo na huingia mkataba wa upangaji. Kadhalika na kodi hulipwa kutegemea na maelewano ya wahusika wenyewe. Pia kumekuwepo na ujenzi wa ...

Read More »

Maji yaunganisha Serikali, upinzani

*Serikali yafungua mlango uwekezaji  katika viwanda *Mbowe ataka elimu, gesi itumike kuzalisha umeme *Zitto apendekeza kodi ya maji Sh 160 kama umeme REA *Wabunge wapendekeza tozo ya maji miamala ya simu Na Waadishi Wetu, Dodoma   Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hii, Serikali na vyama vya upinzani wameungana kifikira kutafuta mwarobaini wa kuondoa umaskini kwa Watanzania. Serikali kwa ...

Read More »

Ndugu Rais nguzo imeanguka paa litashikiliwa na nani?

Ndugu Rais, Abdulrahman Kinana ametuacha! Anataka kupumzika. Mwanadamu ana siku moja tu ya kupumzika. Siku Muumba wako atakayokwita ukasimame mbele ya haki! Siku hiyo utakuwa umelala peke yako! Nawe utakuwa na mapumziko ya milele kwenye nyumba yako ya milele! Hapa duniani pambana na hali yako, Abdulrahman, mahali pa kupumzika hakuna! Ukatibu Mkuu hukuuachia kwa nguvu zako mwenyewe. Tuaminio tunaamini kuwa ...

Read More »

Sudan Kusini kuwekewa vikwazo

JUBA Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limezipa muda wa mwezi mmoja pande hasimu zinazogombana nchini Sudan Kusini kufikia makubaliano vinginevyo nchi hiyo ijiandae kukabiliana na vikwazo. Mchakato huo uliongozwa na Marekani ndani ya Umoja huo ulipata ushindi mdogo wa kura 9 katika baraza hilo lenye nchi wanachama 15 na huku kukionekana na kuwepo kwa hali ya ubishani miongoni ...

Read More »

Bomu la watu laja Afrika – mwisho

Balile

Na Deodatus Balile Mwezi uliopita nimefanya mapitio ya kitabu kiitwacho “Making Africa Work”. Tafsiri isiyo rasmi ya jina la kitabu hiki ni “Mbinu za Afrika kujikwamua kiuchumi.” Kimeandikwa na Greg Mills, Olusegun Obasanjo (Rais mstaafu wa Nigeria), Jeffrey Herbst na Dickie Davis. Kimechapishwa na Taasisi ya Brenthurst Foundation ya Johannesburg, Afrika Kusini. Rais (mstaafu) Benjamin Mkapa ameshiriki uzinduzi wa kitabu ...

Read More »

Ndugu Rais wamekunywa sumu mbona hawadhuriki?

Ndugu Rais waasisi wa nchi zetu hizi tatu, Tanganyika, Kenya na Uganda waliwajengea fikra ya umoja wananchi wake. Tuliopata nafasi ya kufanyakazi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ile iliyovunjika tunaweza kuthibitisha kuwa wananchi sisi na hasa tuliokuwa kwenye mashirika yake tulikuwa wana ndugu pasipo shaka. Watanzania wanaofanyakazi leo katika Jumuiya Afrika Mashariki wana Utanzania zaidi kuliko Uafrika Mashariki. Na Wakenya ...

Read More »

Mbunge apongeza kutimuliwa Dk Machumu

*JAMHURI lilianika ukweli wote likatishwa * CAG amaliza kazi, Mpina apongezwa DAR ES SALAAM NA CLEMENT MAGEMBE Mbunge wa Mafia, Mbaraka Dau amesema amefurahishwa na hatua iliyochukuliwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina kumsimamisha kazi Meneja wa Taasisi ya Hifadhi ya Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU), Dk. Milali Machumu na bodi ya wadhamini wa taasisi hiyo. Dau amesema ...

Read More »

Rais Tserese Khama Ian Khama nguzo ya mafanikio ya Botswana

Na Mkinga Mkinga Aliyekuwa Gaborone, Botswana. Kusini mwa jangwa la Sahara, pamezoeleka kuwa na majangwa kadhaa, ukienda nchini Namibia, utakutana na jangwa la Namib ambalo linakwenda kuungana na jangwa jingine la Kalahari, lililoko nchini Botswana. Nimepata fursa ya ‘kupita’ Botswana mara kadhaa, lakini kipindi hiki nimepata fursa adhimu ya kuitembelea Botswana, kwa siku kadhaa, kutokana na shughuli za kikazi. Hivyo ...

Read More »

Serikali idhibiti ukuaji deni la Taifa

Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad imeangazia mapungufu kadhaa ikiwamo kupanda kwa deni la Taifa. Profesa Assad amewasilisha ripoti hiyo bungeni na kuitolea ufafanuzi kwa umma, kupitia mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika mjini Dodoma. Kwa mujibu wa Profesa Assad, thamani ya sasa ya deni la taifa ni Shilingi trilioni 34.4 wakati ukomo ...

Read More »

Akwilina awe Balozi wa amani

Ijumaa ya Februari 16, mwaka 2017 imekuwa siku ya majonzi kwa taifa letu. Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwiilina B. Akwilini ameuawa kwa kupigwa risasi akiwa kwenye daladala, wakati polisi wanapambana na waandamanaji wa Chadema. Wiki iliyopita nimeandika makala nikitahadharisha juu ya mwenendo wa askari polisi kutumia nguvu kubwa katika masuala ya uchaguzi. ...

Read More »

Tusipuuze tamko la EU

Wiki iliyopita Umoja wa Ulaya umetoa tamko lenye kulitahadharisha taifa letu kuepuka matukio yasiyo na siha njema kwa afya ya taifa. EU wamesema wanafuatia ongezeko la matukio ya kisiasa yenye viashiria vya ukatili na vitisho Tanzania. EU kwa ushirikiano na Mabalozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya wenye uwakilishi Tanzania na kuungwa mkono na Mwakilishi na Mabalozi wa Norwei, ...

Read More »

Tusome ishara za nyakati (3)

Na Pd. Tunda la Kanisa (M.afr)   Wiki iliyopita mwandishi alizungumzia dhana ya kumtegemea Mungu katika kila uamuzi uufanyao kama binadamu. Je, leo unafahamu anazungumzia nini? Endelea… Katika somo la pili mtume Paulo anatuasa kuwa kila mtu afuate wito wake kikamilifu na kutimiza mapenzi ya mwenyezi Mungu. Kama wewe ni padre, sheikh, mchungaji, mwinjilisti, mwanasiasa, mtumishi wa umma, waziri, polisi, ...

Read More »

Ethiopian Airlines wanakula nini?

Na G. Madaraka Nyerere Tumesikia hivi karibuni kuwa kati ya mashirika ya umma ambayo yanapata hasara kubwa ni Air Tanzania Corporation Limited (ATCL), shirika letu la ndege la Taifa. Kwa mujibu wa taarifa ya Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) iliyosomwa bungeni na mwenyekiti wa kamati hiyo, Albert Mtabaliba, ATCL imepata hasara kwa miaka mitatu mfululizo: ...

Read More »

Sababu zinazochangia uchovu mara kwa mara-

Uchovu ni kitu cha kawaida katika maisha ya binadamu. Kila mwanadamu hupitia hali hii na hasa baada ya kupitia shughuli mbalimbali ambazo zilitumia nguvu sana ya mwili au hata akili pia. Ni rahisi sana kuweza kutambua sababu uchovu wa mwili kutokana na shuguli za kila siku. Lakini je? Vipi kwa upande wa mtu yule ambaye anahisi uchovu uliokithiri tena wa ...

Read More »

Uchaguzi Tanzania tutavuna tunachopanda

Balile

Kwa siku za karibuni nimejipa jukumu la kusoma vitabu vitakafitu. Nasoma Biblia na Korani Tukufu. Nasoma maandiko matakatifu. Katika safu hii sitarejea Biblia wala Korani Tukufu, bali ujumbe mmoja tu kutoka vitabu hivi – MAONYO YA MAKUHANI na wengine wanaoitwa manabii kwa njia ya nyaraka. Kila walichokiona walikiandika. Ndiyo maana leo tunasoma Biblia au Korani Tukufu na kupata historia na ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons