Kiungo wa zamani wa Arsenal na timu ya taifa ya Ivory Coast Emmanuel Eboue amepatwa msongo wa mawazo mpaka kufikia hutua ya kutaka kujiua kutokana na hali mbaya inayomkabili katika maisha yake ya sasa.

Eboue alikuwa akipokea kiasi kikubwa katika klabu ya Arsenal huku akipokea zaidi ya £1.5m wakati akiichezea klabu ya Galatasaray.

Eboue amekiri kuwa matatizo yake yalianza baada ya talaka, aliyompa mali zote mkewe Auerilie Bertrand.

Matatizo ya Eboue ya umiliki wa baadhi ya vitu ikiwemo nyumba yake ya kisasa iliyoko London na hana pesa ya kuwalipa watetezi wa kisheria hali ambayo inakaribia kupelekea baadhi ya nyumba na mali alizobakiwa nazo kuuzwa.

Pia ameeleza kuwa sasa hulala sakafuni katika nyumba za marafiki zake na anaishi kwa kazi ndogo ndogo mitaani, na kuiomba Arsenal na yeyote mpatie msaada.
Kutokana na msongo wa mawazo mkubwa unaochangiwa na kuzuiliwa kuwatembelea watoto wake watatu Mathis, Clara na Maeva katika msimu huu wa Xmass.

1797 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!